EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 15, 2012

‘Wabunge wanaosinzia wachapwe viboko’

WAKAZI wa Kata ya Misalai Tarafa ya Amani Wilayani hapa, wamependekeza kuwepo kwa kipengele cha adhabu ya kumwagiwa maji ya baridi na kisha kuchapwa viboko kwa mbunge atakayesinzia akiwa kwenye kikao bungeni.

Wamependekeza pia kwamba adhabu hiyo iambatane na kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo pamoja na kuzuiwa kugombea tena kipindi kingine mara
muda wake utakapomalizika.

Walitoa mapendekezo hayo kwa wajumbe wa Tume ya maoni ya marekebisho ya Katiba ilipofika Kijiji cha Misalai kukusanya maoni ya wananchi wa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza.

Shukrani Said (23) ambaye ni mkulima wa Kijiji cha Ziarai Kata ya Misarai wilayani hapa alisema kutokana na baadhi ya wabunge kuonekana mara kwa mara kupitia runinga inayoonyesha vikao vya Bunge kuonekana wakiwa wamesinzia kuna kila haja ya Katiba mpya kuwekwa vifungu vitakavyowabana wasilale bungeni.

“Wabunge hatukuwatuma waende wakalale, matokeo yake zinapitishwa sheria zinazotubana, tuliwachagua waende wakatuwakilishe, kwa hiyo kuwe na kipengele cha adahabu ya viboko,” alisema Shukrani na kusisitiza kuwa
adhabu hiyo inavyofanyika ionyeshwe kwenye runinga.

Richard Lutangilo wa Kijiji cha Bulwa Wilayani hapa alisema pamoja na adhabu ya viboko, Katiba iongeze kipengele cha kumwagiwa maji kila mbunge atakayesinzia na kama haitoshi asipewe ruhusa ya kuhudhuria vikao vitatu mfululizo na pia asiruhusiwe kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo mara kipindi chake cha miaka mitano kinapomalizika.

“Hili la viboko likiwekwa kwenye Katiba litaleta umakini wa wabunge wetu kwani tunawaona inatuhuzunisha sana sisi wapiga kura tunapowaona wakiwa wamelala fofofo bungeni wakati vikao vikiendelea,” alisema Jackob
Zephania.

Hadi Mlowe (50) mkazi wa Kijiji cha Mgambo Wilayani hapa alipendekeza umri wa wagombea wa nafasi ya ubunge uanzie miaka 45 kwa kuwa amebaini wabunge vijana ndiyo chanzo cha kukosekana kwa nidhamu ndani ya Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Napendekeza katiba mpya iweke ukomo wa umri wa kuanzia kwa nafasi ya ubunge ili kuondokana na chombo hiki muhimu kukosekana kwa nidhamu tunasikia jinsi wabunge vijana wanavyoropoka linaonekana kama ni Bunge
la kihuni,” alisema Mlowe.

Cleopas Mutabuzi (50) mkulima wa Kijiji cha Misalai alipendekeza madaraka ya Rais yapunguzwe hasa katika kuteua mawaziri, ambapo alitaka waajiriwe na Tume ya Utumishi kwa kufuata taaluma zao na siyo
kuchaguliwa kisiasa.

Kadhalika nafasi ya Spika, naibu Spika na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipendekeza zisitokane na wabunge bali waajiriwe kupitia Tume ya Utumishi na baadaye majina yao yapitishwe bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na wabunge.

Kamati hiyo ya kupokea maoni ya marekebisho ya Katiba  ilikuwa wilayani hapa kwa muda wa siku tatu ambapo
iliendesha mikutano Majengo, Kwafungo, Mkuzi, Misozwe, Amani na
Misalai. 
Habari na Burhani Yakub, Muheza.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate