Watoto
watatu wa familia moja wamewafikisha wazazi wao katika Kituo Kikuu cha
Polisi mjini Musoma , Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto wakidai
kutelekezwa na kuwafanya kuishi maisha ya kutangatanga mitaani ilhali
wazazi wao wakiendelea na maisha yao bila ya kuwajali.
Wakizungumza nje ya kituo hicho cha Polisi, mmoja wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina la Justine Kichere alisema baba yao mzazi kwa kushirikiana na mama yao wa kambo ambaye hawakuweza kumtaja jina lake, waliwafukuza nyumbani kwa kuwatupia nguo zao kwa kile walichokieleza kudaiwa kuwa 'machokoraa’, yaani watoto wa mitaani.
Wakielezea chanzo cha tukio hilo la kufukuzwa nyumbani, Justine (14) anayesoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Rwamlimi A katika Manispaa ya Musoma, alisema waliitwa na mama yao wa kambo akiwa na wadogo zake, James (13) na Gerald (12) na kuelezwa kuwa mama yao anaumwa na amelazwa Hospitali ya Mkoa, hivyo waende kumjulia hali.
Aliongeza kuwa, wakiwa njiani kuelekea hospitalini huku wakiwa hawapajui waliomba msaada katika gari moja na kueleza wanakwenda hospitali ya Mkoa na kupandishwa kisha kuelekea wasipokujua na walipofika na kuuliza waliambiwa wapo maeneo ya Ramadi.
Alidai baada ya kudaiwa kupotea, waliomba msaada wa kurudi nyumbani Musoma na kusaidiwa lakini mara baada ya kufika nyumbani bila kuulizwa kilichowasibu walitupiwa nguo zao nje na kutakiwa kuondoka nyumbani na watafute mahala pengine pa kuishi.
Justine alisema baada ya kufukuzwa na baba yao pamoja na mama yao wa kambo waliamua kwenda kwa mama yao ambaye alitengana na baba yao anayeishi maeneo ya Baruti na kukaa kwa muda wa siku mbili kisha mama yao kuwataka kurudi kwa baba yao kwa kuwaeleza kuwa, hana pesa ya kuwalisha wote watatu.
Kwamba, baada ya kuona hawana pa kwenda, waliamua kuishi mtaani kwa takribani wiki moja huku wakiwa wakilala katika jumba bovu eneo la Nyakato, lakini baada ya kuona maisha yakiendelea kuwa magumu, waliamua kwenda kituo cha Polisi ili kuweza kupata msaada zaidi.
Mtoto huyo aliongeza kuwa hilo sio tukio la kwanza kwa baba yao Kichere Sangi aliyemueleza kuwa ni mfanyabiashara wa duka la rejareja katika maeneo ya Kigera kufanya hivyo kwa kuwa alishawahi kumfukuza kaka yao, Geofrey Kichere aliyekuwa akisoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Bweri ambaye mpaka sasa hajulikani halipo.
Aidha watoto hao walisema lengo la kwenda katika kituo cha Polisi ni kutaka kupata msaada kwa kuwa maisha wanayoishi mtaani ni magumu na wameshindwa kwenda shuleni huku mmoja wao akiwa anakabiliwa na mtihani wa darasa la saba
Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi ya dawati la jinsia na watoto katika kituo cha Polisi Musoma kutaka kujua hatima ya watoto hao na kuelezwa kuwa wanazo taarifa hizo na hatua waliyochukua ni kundika barua wa wito kwa wazazi ili kuelezea madai ya watoto hao.
HabariLeo

No comments:
Post a Comment