Magoli
mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza
katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika
dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe
la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa
goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Tanzania
ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya
Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa
michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa
katika hatua ya robo fainali.
Yanga
pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na
Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji
kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.
No comments:
Post a Comment