EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 24, 2012

ZITTO AREJESHA PENZI LA WEMA, DIAMOND







Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu.

Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.
Diamond na Wema, walinaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.
SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.

Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.
WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA?
Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.
Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.
HAKIKA WANAPENDANA
Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa!

Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema.
‘Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.

Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi.
Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.
RAHA NDANI YA TILAPIA HOTEL
Safari ya furaha kwa Wema na Diamond, ilihamia ndani ya Jiji la Miamba ya Mawe, Mwanza ‘Rocky City’ kwenye Hoteli ya Tilapia, iliyopo ufukweni mwa Ziwa Victoria, eneo la Capri Point, hiyo ikiwa Julai 19, 2012.

Habari zinapasha kuwa wawili hao, walipumzika kwenye hoteli hiyo kwa muda mfupi, wakati wanasubiri saa ya ndege yao ya kuwatoa Mwanza hadi Dar es Salaam ifike.

Ndege waliyopanda Diamond na Wema kutoka Kigoma, ilitua Mwanza saa 9:30 alasiri, hivyo kuanzia muda huo, waliutumia Tilapia Hotel mpaka saa 2:30 usiku, wakaripoti Uwanja wa Ndege wa Jiji la Miamba ya Mawe, kabla ya saa 3:50 usiku, usafiri huo wa anga, uliitupa mkono ardhi ya Mwanza mpaka Dar es Salaam.
AIR PORT DAR ES SALAAM
Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra Sammi’, alionekana Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kuanzia saa 4:45 usiku (Julai 19), hivyo kwa jicho la ripota wetu, ikawa wazi kwamba amekwenda hapo kumpokea mwanaye kipenzi, Diamond ‘Sukari ya Warembo’.

Kutokana na safari hiyo kuwa mguu wa Diamond uliambatana na wa Wema, kwenda kwenye shoo ya kutoa shukurani nyumbani kwao Kigoma, ni wazi Mama Nasibu (Mama Diamond) alikuwa pale pia kwa minajili ya kumlaki mkwe a.k.a Mka Mwana.
PW 415 YAWASILI DAR
Diamond na Wema, walipanda ndege ya Kampuni ya Precision Air, PW415 na ilipotimia saa 5:30 usiku, ilitangazwa kuwa ndiyo inawasili kwenye uwanja huo wa ndege wenye jina la muasisi wa taifa huru la Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ‘Baba wa Taifa’.
Milango ya saa 5:52, Diamond na Wema, walipita kwenye mlango wa wanaowasili (arrivals gate), wakiwa sambamba na Ommy Dimpoz, walipokelewa na Mama Nasibu hadi sehemu ya maegesho ya magari uwanjani hapo.

Timu nzima, ilijipakia kwenye gari la Diamond aina Toyota Land Cruiser Prado, rangi ya fedha, wakatoweka eneo la uwanja huo.
DIAMOND KWA WASIWASI
Saa 6:14 usiku (Julai 20), Diamond alimpigia simu ripota wetu, eti akahoji kilichompeleka uwanja wa ndege. Mahojiano yalikuwa hivi;
DIAMOND: Kiongozi nilikuona Air Port, pale ulikuwa unafanya nini?
RIPOTA: Aah, kumbe uliniona? Mlivyojikausha nikadhani hamkuniona. Kuna mzigo wangu nilikuwa naufuatilia pale.
DIAMOND: Mzigo wapi? Naomba uniambie ukweli.
RIPOTA: Acha hizo dogo, unafikiri mimi nilikufuata wewe? Tena ningejua unafika leo, halafu ujio wenyewe ni huo, ningetega kamera zangu na tuwapige picha za kutosha.
DIAMOND: Aah, usifanye hivyo kiongozi.
Baada ya mazungumzo hayo, Diamond kila alipopigiwa simu hakupokea mpaka gazeti hili linanyanyuka kwenda kiwandani.
UFAFANUZI WA WEMA
Wema alipopigiwa simu na ripota wetu, alijibu kuwa yeye na Diamond hawajarudisha mapenzi, isipokuwa hivi sasa wako karibu kama marafiki wazuri kwa ajili ya kusaidiana mambo mbalimbali.
“Kusema ukweli kwa sasa sijafikiria kurejesha mapenzi na Diamond ila tupo karibu kama marafiki,” alisema Wema.
ZITTO NAYE
Jitihada za kumpata Zitto aweze kuzungumzia kurejea kwa penzi la Wema na Diamond kwenye tamasha aliloliandaa, hazikuzaa matunda. Muda wote naibu huyo wa Kambi ya Upinzania Bungeni, simu yake ilikuwa imezimwa.
WANANCHI WAMPONGEZA
Fununu kuwa Wema na Diamond wamerudiana zilivuma kwa kasi ndani ya mitandao ya kijamii na maoni ya wengi yakaelekeza pongezi kwa Zitto, kwani kabla ya hapo, mastaa hao walikuwa na uhasama mkubwa.
UNAKUMBUKA?
Malumbano yao kwenye vyombo vya habari? Diamond alipomfedhehesha Wema baada ya kukataa kupokea fedha zake alizomtuza kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Machi mwaka huu? Je, kauli nzito za Mama Wema, Mariam Sepetu kwamba Diamond ni kijana mbaya na hafai?
JIULIZE SASA
Mpaka hapo bado unabisha kwamba mapenzi ni upofu? Unaendelea kukataa kwamba mapenzi hayaulizwi kwa nini? Diamond alipoachana Wema, alitua kwa Miss Tanzania namba mbili 2006-07, Jokate Mwegelo, je, penzi lao limeyeyuka au bado lipo kwa sura gani?

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate