Joyce Mwasilombe mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi ya sabena akisimulia mkasa huo. |
WATU 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa
wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania
lenye namba T570 AAM lililokuwa limejaza kupita kiasi kupata ajali na kupinduka.
Basi hilo lilikuw alikitoka tabora kwenda Mbeya
miguu juu |
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda
wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Miongoni wa watu waliokufa ni watoto
watano, wanawake sita na wanaume sita na kwamba hadi leo mchana, miili ya watu
saba ilikuwa imetambuliwa akiwemo askari Polisi, Konstebo Kheri wa Kituo Kikuu
cha Polisi mjini Tabora.
Wengine ni Vitus Tulumanye, Farah Inga (Mzimbabwe),
Ikamba Thadeo, Damalu Goma, Beatrice Kalinga , Andrew Madirisha . maiti
zilizobaki zipo hospitali ya Kitete zikisubiri utambuzi..
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony
Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa
na abiria zaidi ya 100.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Antony Rutta akitoa maelezo ya ajali kwenye eneo la tukiokwa waandishi wa habari. Via http://lukwangule.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment