EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, August 5, 2012

Amwua mwanaye kwa "kero ya kuchekwa" na watu kuwa amezaa na mlemavu

MKAZI wa kijiji cha Mubinyange, Ngara, mkoani Kagera, Adam Balekawe (32), anadaiwa kufanya mauaji ya kinyama, kwa kumchoma sindano ya sumu na kumnywesha sumu mtoto wake mwenye umri wa wiki tatu Amani Adam, akihofia kuchekwa na ndugu kwa kuzaa na mwanamke mwenye ulemavu.

Kutokana na tukio hilo la hivi karibuni, Balekawe ametiwa mbaroni na juzi alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ngara kusomewa mashitaka ya mauaji. Hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na hivyo kurudishwa rumande.

Ilidaiwa kuwa, kabla ya kukamatwa Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi, mshitakiwa alikuwa anakusudia kutorokea nje ya nchi.

Akisimulia tukio hilo nje ya mahakama, mama wa mtoto aliyekufa, Ombeni Paschal (27) alidai kuzaa mtoto huyo kwa njia ya operesheni, baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.

Alidai kuwa siku ya tukio mzazi mwenzake huyo alimtembelea saa nne usiku na kumkuta amelala chumbani na mtoto aliyekuwa na afya njema, ambapo alishangaa kumwona amesimama pembeni mwa kitanda akimwangalia, “Alifika usiku, nilishituka kumwona amesimama pembeni mwa kitanda, nikamsalimia, lakini wakati huo alikuwa akinimulika na tochi ya simu machoni, kisha akaniomba nimpe mtoto ambebe, nikamvisha mtoto nguo za baridi akamchukua na kutoka naye sebuleni,’’ alidai Ombeni na kuongeza: “Ghafla nilisikia mtoto akilia kwa sauti mara tatu kama vile amepatwa na kitu, nikashituka, wakati nafanya jitihada za kushuka kitandani na hasa ukizingatia hali yangu ya ulemavu niliyonayo hii, akaingia chumbani akimleta mtoto akaniambia nimnyonyeshe, lakini wakati huo mtoto akawa amepanua midomo huku akitokwa na povu mdomoni’’.

Alidai, alipoulizwa kilichomsibu mtoto mpaka kulia hivyo na kutokwa na povu midomoni, alisema hajui, “kisha akachukua Sh 15,000 akanitupia kitandani na kuniambia anakwenda kutafuta chakula, kwa sababu alikuwa hajala. Baada ya kunitupia pesa kitandani, aliondoka, nikamchukua mtoto kumnyonyesha akawa hata hawezi kunyonya huku akitokwa na povu na kujiharishia, hali ambayo ilinichanganya na kunifanya nipige kelele za kuomba msaada kwa majirani ambao walifika mara moja chumbani kwangu,’’ alifafanua Ombeni.

Huku akitokwa machozi, Ombeni ambaye ni mlemavu anayetembea kwa magongo, alidai kuwa baada ya majirani kuona hali hiyo ya mtoto walimchukua na kumkimbiza hospitalini, lakini walipofika nje ya nyumba mtoto alikata roho.

“Alikatia roho hapo mlangoni kwa sababu walipoona hali yake ni ya kutisha na hasa mtoto ambaye alikuwa mzima wa afya njema kabisa na hasa siku hiyo ambapo alikuwa akionekana mchangamfu sana, mimi nilikuwa najiandaa ili niwafuate hospitalini lakini ghafla majirani wakarudi ndani wakaniambia mtoto amekufa.

Alidai kuwa tangu alipomweleza mwanamume huyo ambaye amekuwa naye kimapenzi kwa miaka mitatu kwamba ana ujauzito, alibadilika tabia huku akimtaka kuutoa ujauzito huo kwa madai kuwa hayuko tayari kuzaa naye mtoto, kwani amekuwa akichekwa na marafiki na ndugu zake kwamba ‘anatembea’ na mlemavu.

Alisema alikataa, lakini siku moja aliugua na kumweleza mwanamume huyo ambaye alikwenda kumnunulia dawa na kumtaka aimeze, na baada ya hapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Murugwanza ambapo ilibainika kuwa alimeza vidonge vya kutoa mimba, hata hivyo alisema madaktari walifanya jitihada za kuhakikisha kwamba wanaokoa maisha yake na ya mtoto tumboni.

Alibainisha kuwa wakati wote wa ujauzito, mwanamume huyo alikuwa akimweleza kwamba ameanza kuchekwa na ndugu na marafiki kwamba amezaa na mlemavu, akisisitiza kuwa hawakuwa na makubaliano ya kuzaa mtoto, bali kufanya mapenzi tu.

Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa mtoto huyo, Dkt. Raphael Rwezaula alithibitisha kuwa chanzo cha kifo ni sumu, hata hivyo hakutaja aina ya sumu na kueleza kwamba itapelekwa kwenye maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo ili kubaini aina ya sumu iliyomwua.

Alisema vipimo vimeonesha kwamba sumu hiyo iliingia mwilini kwa mtoto kwa sindano na kunyweshwa. Kutokana na hali hiyo, Dkt. Rwezaula alilazimika kukata baadhi ya vipande vya nyama kutoka mwili wa mtoto huyo shingoni na tumboni, na tayari vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini sumu hiyo.

via HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate