ILE kasumba kwamba hakuna msanii wa bongo muvi anayeweza kuolewa na kudumu ndani ya ndoa, inatarajia kufutwa na msanii Aunty Ezekiel, ambaye
anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi
wake anayeishi Dubai ambako ndiko atakoenda kuishi baada ya kufunga
ndoa.
Aunty Ezekiel mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood balozi wa Zuku Swahili movie.
Aunty Ezekiel
alisema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka
kufunga ndoa kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye
maisha.Alidai kuwa mpenzi wake huyo ni Mtanzania ingawa anaishi nje, ambapo
anaamini baada ya kufunga ndoa na yeye anataweza kwenda kufanya
kazi huko.
Aunty Ezekiel akiwa katika kurekodi moja ya filamu zake.
Aunty Ezekiel akiwa katika kurekodi moja ya filamu zake.
“Nilikuwa kimya juu ishu hii lakini nachotaka kusema ni kwamba mambo
yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu
nahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua kuchukua maamuzi hayo,”
alisema.
Ezekiel alisema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa.Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

No comments:
Post a Comment