MKAZI wa Kigogo jijini Dar es Salaam, Joseph
Semwenda (42) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Sokoine Drive akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kumiliki na
kuendesha maabara bila ya kuwa na usajili. Semwenda alifikishwa
mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yanayomkabili mbele ya Hakimu
Timoth Lyon.
Mwendesha Mashitaka Mkuu, John Kijumbe alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Julai 27, mwaka huu saa 5:00 asubuhi katika eneo la Kigogo, Wilaya ya Kinondoni, Semwenda alikamatwa na Mratibu wa Hospitali Binafsi wa manispaa ya Kinondoni, Alfred Ngowi akiendesha huduma za maabara ya matibabu bila ya kusajiliwa.
Kijumbe alidai kuwa siku hiyo mshitakiwa alikamatwa na Ngowi akitoa huduma za vipimo vya maabara bila ya kuwa na ujuzi.
Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika waliotakiwa kusaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja. Kesi hiyo itatajwa tena Agosti, 14 mwaka huu.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment