WAUGUZI wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kughushi vyeti
na kuwasilisha nyaraka za uongo kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga
nchini.
Washitakiwa walisomewa mashitaka mbele ya Mahakimu wawili tofauti ni Atupenda Lyandala (35) na Mwanaidi Hemed (30).
Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agness Mchome kuwa, muda na siku isiyofahamika, Mwanaidi alighushi cheti cha usajili wa uuguzi chenye namba 25099 cha Agosti 28, 1996 akidai kimetolewa na Baraza la Wauguzi na Wakunga nchini.
Alidai kuwa, Mei 31 mwaka huu katika Ofisi za Baraza la Wauguzi na Wakunga nchini, Mwanaidi aliwasilisha cheti hicho kwa Gustavo Moyo huku akijua ni cha kughushi.
Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Agosti 14 mwaka huu, kesi itakapotajwa tena.
Katika hatua nyingine, Wakili wa Serikali Hamis Tesha alidai mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana kuwa, muda na siku isiyofahamika, Atupenda alighushi cheti cha usajili wa uuguzi chenye namba 38572 cha Septemba 2007 akidai kimetolewa na Baraza la wauguzi na wakunga nchini jambo ambalo si kweli.
Aliendelea kudai kuwa, Mei 28 mwaka huu katika ofisi za baraza hilo, Atupenda aliwasilisha cheti hicho kwa Jane Msiru huku akijua kuwa ni cha kughushi. Katika mashitaka mengine ilidaiwa kuwa, Atupenda alighushi cheti namba 22134 akidai kimetolewa na baraza hilo na kisha kukiwasilisha kwa Msiru huku akijua ni cha kughushi.
Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Agosti 14 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment