Casting Coordinator wa ALLY REHMTULLA'S COLLECTION 2012 Audition Martin
Kadinda akitoa mwongozo wa zoezi hilo kwa Models walioshiriki.
Baadhi ya Models wa kiume waliojitokeza Serena Hotel wakisubiri usaili.
Pichani Juu na Chini ni Models wa kike na wa kiume wakipita mbele ya Majaji wakati wa usaili.
Meza kuu ya Majaji kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Alliance Auto Bw.
Alfred Minja akiwakilisha CFAO Motors wauzaji wa Magari ya Mercedes Benz
ambao ndio wadhamini wakuu wa 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013', Aysha
Mbarak Meghji kutoka Ayman Garage-Convolution Ideas Ltd, Administrative
Assistant Mawalla Advocate na pia ni Model Myler Nyangasa, Mwasisi na
CEO wa Missie Popular Blog Mariam Ndabagenga na Fashion Stylist wa
Fashionnjukii.com Rosemary Kokuhilwa.
Pichani Juu na Chini Models wa kike wakionyesha umahiri wa Catwalk
wakati wa Audition kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki "ALLY
REHMTULLAH COLLECTION 2013".
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Models wa kiume wakipita jukwaani mbele ya majaji.
Baadhi ya Models wakiwa katika tafakari ya SIJUI NITAPITA wakati wa
usaili huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed ambao ni wauzaji wa magari
aina ya Mercedes waliodhamini onyesho la 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION
2013' akielezea kuwa Mercedes Benz imedhamini Onyesho hilo kwa mara ya
kwanza kwa sababu kwanza wanamkubali Ally Rehmtullah kama mmoja wa
wabunifu wenye hadhi ya juu hapa nchini na kuwa wamechagua Brand ya
Mercedes Benz kwa sababu ni magari yenye kiwango cha juu na Rehmtullah
ana ubunifu wa hali ya juu.
Mercedes Benz imekuwa ikijihusisha na udhamini wa 'High and Fashion
Show' duniani kote pia Orchestra, Baley na Sailing matukio ambayo
yanaendana na hadhi ya magari ya Mercedes. Kulia ni Chief Editor wa MO
BLOG Lemmy Hipolite.
Sales & Marketing Representative kutoka RAHA Preetkamal Bansal
akielezea kuwa kampuni yake imekuwa na furaha kushirikiana na Ally
Rehmtullah kwa kuwa ubunifu wake ni wa hali ya juu kama wao wanavyotoa
huduma za Intaneti za hali ya juu na wamekuwa wakitoa huduma ya ISP
(Internet Service Provider) kwa muda wa miaka 16 kwa kiwango kilekile.
RAHA wakiwa wadhamini muhimu watawezesha watu kuona Live 'ALLY
REHMTULLAH COLLECTION 2013' itakayofanyika September 8 mwaka huu ambapo
Watu duniani kote wataona kupitia www.ar.co.tz
Amemalizia kwa kusema "On the day the Jungle puts on its show Our Broadband let you watch it Live".
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quality Furniture Limited Bw. Mahad A Nur
akisema wameamua kujihusisha kudhamini show hii ya Ally Rehmtullah ili
kutoa ufahamu kwa umma juu ya ubora wa bidhaa wanazotengeneza na siku ya
Onyesho hilo watatoa Furniture zitakazotumika sehemu ya wageni maalum
(VIP).
Quality Furniture Limited wanatengeneza bidhaa zenye Quality kama
lilivyojina lao na kama ilivyo show ya Ally Rehmtullah lakini pia Bw.
Mahad amesema wako tayari kuwadhamini wabunifu chipukizi watakaokuja na
ubunifu wenye Quality.
Majaji Aysha Mbarak Meghji na Rosemary Kokuhilwa wakibadilishana mawazo
baada ya kazi kubwa ya kuchagua Models watakaoshiriki 'ALLY REHMTULLAH
COLLECTION 2013'.
Ally Rehmtullah.
No comments:
Post a Comment