NIPASHE -- Katika
kuhakikisha kampeni ya umeme vijijini inafanikiwa, Shirika la Umeme
Tanzania (TANEESCO) limeanza kusambaza kifaa kinachotumika ndani ya
nyumba ambacho hakihitaji nyumba kufungwa nyaya (wiring).
Kifaa hicho kinachojulikana kwa jina la Ready Board au Umeme Tayari (UMETA), kinatoa unafuu mkubwa kwa mteja.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu matumizi na unafuu wa kifaa hicho, Ofisa Mwandamizi Masoko wa TANESCO, Joseph Chilambo, alisema mteja atalazimika kununua kifaa hicho kwa Sh. 42,480 na kisha kulipia gharama za kuunganishiwa umeme, “Sisi TANESCO tukija kwa mteja tunamuunganishia umeme na hiki kifaa, wala hahitaji kufanyiwa wiring, tukisha mpachikia kifaa hiki atakua na uwezo wa kutumia friji, tv, radio, hata mashine ndogondogo kama za kuunganishia vyuma (welding),” alisema.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo, kifaa hicho ni mahususi kwa nyumba ya vyumba angalau viwili na sebule au chumba kimoja cha biashara au ofisi. Alisema mara nyingi wamefanikiwa kuunganisha kifaa hicho vijijini kupitia Mradi wa Mamlaka ya Usambazaji Umeme Vijijini (REA) ambapo kupitia mradi huo, mteja atalazimika kulipia sh. 117,000 ikiwa ni gharama za kuunganishiwa na kulipia kifaa hicho, “Unajua kifaa hiki kitapunguza malalamiko mengi yanayosababishwa na mafundi mchundo wa TANESCO (Vishoka), hawa wamekuwa wakiwalaghai sana wateja wetu lakini kwa kifaa hiki, utapeli huo utakoma hasa vijijini,” alisema Chilambo.
Kwa mujibu wa Chilambo, kufanya wiring nyumba yenye vyumba kati ya viwili na vitatu ni kati ya sh. 500,000 na 700,000, lakini kwa kutumia kifaa hicho, mwananchi wa kijijini atatumia sh. 117,000.
Read Board ni kifaa kilichoundwa kikiwa na swichi kubwa (main switch) ikiwa na kikata umeme (circuit breaker), taa moja na soketi tatu za swichi. Katika soketi hizo tatu, ya kwanza kushoto ni kwa ajili ya vifaa vinavyotumia umeme mwingi kama vile jiko, ya kati ni kwa ajili ya vifaa vya umeme mwingi kiasi kama pasi na ya tatu ni kwa ajili ya umeme mdogo kama radio, tv na feni.
Naye fundi wa TANESCO aliyeko Idara ya Masoko anayehusika na kusambaza kifaa hicho, Mussa Chowo, alisema soko lao kubwa liko vijijini. Aliitaja mikoa ambayo kifaa hicho kimefungwa kwa wingi kuwa ni Kigoma, Tabora, Mwanza, Manyara, Simiwi na Kagera.
Kifaa hiki kimetengenezwa Afrika Kusini na kimefanyiwa majaribio na mamlaka zote za kuthibitisha ubora. Pamoja na unafuu wa kutumia kifaa hiki katika kuingiza umeme nyumbani, lakini shirika hilo bado halijakitangaza kwa kina.
Hata hivyo, maofisa waandamizi wa shirika hilo wamekiri kuwa pamoja na kuwa kifaa hicho kimeanza kutumiwa nchini kwa zaidi ya miaka mitano sasa, lakini Watanzania wanaokielewa na umuhimu wake ni wachache sana.

No comments:
Post a Comment