EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 10, 2012

Changamoto katika huduma za afya: Bahi wajifungulia nyumbani kukwepa wauguzi ‘watoto’

Asilimia 25 ya wajawazito katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma bado wanajifungulia nyumbani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutotaka kuzalishwa na wauguzi wenye umri mdogo kuliko wao.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Ntuli Kapologwe alisema hayo juzi mjini hapa katika mahojiano na gazeti hili (HabariLeo). Alisema kuwa wanaendelea na kampeni ya kutoa elimu ili wajawazito waone umuhimu wa kujifungulia hospitali na si majumbani kama wanavyofanya, “Wengi bado wana mila na desturi kuamua kujifungulia nyumbani kwa vile watumishi wanaowazalisha wana umri mdogo na wengi wanaona binti mdogo hawezi kumzalisha,” alisema.

Pia alibainisha kuwa mwaka 2010 kulikuwa na vifo saba vilivyotokana na uzazi na mwaka 2011 kulikuwa na vifo viwili na kwa mwaka huu mpaka sasa kuna kifo kimoja tu kilichotokana na uzazi.

Alisema hayo ni moja ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na kuboreshwa kwa huduma za afya katika wilaya hiyo uliochangiwa kuwepo kwa mfumo mzuri wa rufaa ambapo vituo vinne vya afya vina magari ya kubebea wagonjwa. Vituo hivyo ni Bahi, Mundemu, Chipanga na Mtitaa.

Dkt. Kapologwe alisema kuwa Kituo cha Afya cha Chipanga kina huduma ya upasuaji ya uzazi wa dharura na watumishi wamekuwa wakipewa motisha ambapo watumishi wanaoishi mbali na vituo vya kazi wamepewa usafiri wa pikipiki, “Mwaka huu tutafungua zahanati mpya mbili katika Kijiji cha Mindola Kata ya Ilindi na Kijiji cha Magaga Kata ya Chifutuka,” alisema.

Dkt. Kapologwe alisema bado kwenye baadhi ya maeneo wananchi wanaamini kujitibia majumbani ndiyo njia bora kwani wengi bado wana imani za kishirikina ambapo wameendelea kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kupambana na maradhi.

Pia alibainisha kuwa Wilaya hiyo bado haina hospitali ya Wilaya na wamekuwa wakiomba wafadhili na hata Serikali kuwezesha wilaya hiyo kuwa na hospitali ambapo mpango wa kujenga umeanza na eneo tayari limepatikana.

via HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate