MTAYARISHAJI
wa filamu Swahiliwood William J. Mtitu ambaye anatarajia kufunga ndoa
mwisho mwa mwezi wa nane na mpenzi wake ambaye amekataa kumtaja kwa
jina, anasema kuwa harusi yake itakuwa ni harusi ya kihistoria kwani
itakuwa tofauti kabisa na harusi za wasanii wote zilizowahi kutokea
katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mtitu mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood.
“Nashukru kampani ninayopata kutoka kwa wasanii wenzangu kutoka Bongo
movie Unity na wadau wengine wa filamu kwa ujumla, pamoja na vikao
kuendelea lakini kuna kitu ambacho tunatarajia kukifanya, kitu hicho
katika harusi hii hkutakuwa na mtu yoyote atayevaa suti kama
ilivyozoeleka katika harusi nyingine,”anasema Mtitu.
Mtitu akiwa na mkewe mtarajiwa .
Pamoja
kuongea hivyo lakini mtayarishaji na mwigizaji wa filamu huyo hakusema
kuwa wageni waarikwa na maharusi watavaa nguo za aina gani katika
sherehe za harusi hiyo na kusema kuwa wapo katika mipango ya kuchagua
vazi ambalo si suti na ikiwa tayari atawajulisha wadau wote
watakaoarikwa katika harusi hiyo.
No comments:
Post a Comment