EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, August 5, 2012

Machache yaliyozungumzwa Magic FM jana: Zitto na Urais; Masha na Ubunge

Akizungumza katika kipindi cha Makutano kinachorushwa an redio ya Magic FM ya jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) alisema suala la kugombea urais ni azma yake kutoka moyoni na kueleza kuwa yeye ni tofauti na wanasiasa wengine ambao hulitaka jambo kwa kisingizio cha kutumwa na watu wengine.

Hata na hivyo, mwanasiasa huyo machachari hakuweka wazi mwaka wa uchaguzi ambao atagombea urais kama ambavyo amekwisha kutangaza, “Ni kweli nautaka urais jambo ambalo nataka Watanzania wajue, mimi sikusema ni lini lakini nia yangu ipo…iwe mwaka 2015, 2020 au 2025. Dhamira yangu nataka siku moja kuliongoza taifa langu, kama mwanasiasa mkomavu huu ni uamuzi wangu kutoka moyoni, sijatumwa wala kuagizwa na mtu yeyote. Siamini katika kauli za kutumwa, kuombwa wala kuagizwa ila kwa mwanasiasa anayejiamini katika uongozi lazima athubutu kuweka dhamira ya kweli katika kuongoza wananchi,”alisema Zitto.

Zitto alisema pamoja na dhamira yake hiyo, ataendelea kufuata sheria na taratibu ambazo ni pamoja na kupata ridhaa ya chama chake cha CHADEMA.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema hadi hivi sasa chama chake hakina mgombea urais na kueleza kuwa muda ukifika suala hilo litakuwa bayana.

Zitto alisisitiza kuwa hana ubinafsi juu ya hoja hiyo na kusema kuwa mwanachama yeyote atakayeteuliwa kupeperusha bendera katika wadhifa huo yuko tayari kumuunga mkono.

Akizungumzia suala la tuhuma za rushwa linalohusisha wabunge kuhongwa na kampuni na baadhi ya makampuni ya mafuta, Zitto alirejea msimamo wake wa kupinga kuhusika katika rushwa.

Zitto alisema binafsi yake anaiamini tume iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika kushughulikia sakata hilo kwa kusema kuwa ripoti ya tume hiyo itabainisha ukweli iwapo anahusika au la, “Kwa sasa tumekuwa katika taifa la majungu, uwongo, fitna na tuhuma zisizokuwa na maana na haya yamekuwa kama maisha ya kawaida ya wananchi. Nadhani kwa hili tusiliongelee sana na tuiachie tume iliyoundwa kuchunguza jambo hili ifanye kazi kwa uhuru mkubwa..kwani inatakiwa kutoa majibu yake ndani ya siku 14…msihofu majibu yatatoka tu hivu karibuni,”alisema Zitto.

Zitto pia alisisitiza kuwa yeye siyo mla rushwa na wala hajawahi kula rushwa.


Mwanasiasa huyo kijana anadaiwa kuwa na utajiri mkubwa na baadhi ya mali anazodaiwa kuwa nazo ni pamoja na ujenzi wa kasri unaoendelea Mbezi Dar es Salaam na magari ya kifahari.

Katika mahojiano hayo, Zitto alikanusha madai hayo akisema maneno yote hayo yaliyoibuka ni fikra hasi juu ya nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), “Dhamana niliyonayo katika POAC inawajenge watu sura tofauti ya labda najinufaisha na madaraka yangu katika kamati hiyo…nasimamia mashirika zaidi ya 290, kwa hiyo wanafikiri Zitto ni tajiri.Na kama vile haitoshi ule msimamo wangu kupinga posho za ubunge nayo ilifanya wengi wachukie …lakini nitaendelea na msimamo wangu ule ule. Kuhusina na mali zangu ..mimi si tajiri kama wengi wanavyodhani, sina Range Rover, Hammer au jumba la fahari kama watu wanavyozusha. Mimi ninajenga Kigoma, Dar es Salaam sina nyumba, sina kiwanja achilia mbali kiwanja sijawahi kuomba kiwanja Dar es Salaam wala Dodoma, hilo kasri nitakuwanalo wapi?. Nakumbuka siku hiyo mambo haya yaliibuka ilikuwa siku ambayo bajeti ya Nishati na Madini ilikuwa inawasilishwa ….na katika wakati mwengine siku hiyo hiyo, mishahara na posho mpya kwa wabunge zilianza kutoka, hivyo basi wabunge wengi walichangia jambo hilo hadi wengine wasiopenda kuzungumuza siku hiyo walizungumza,” alisema Zitto.

Alipohojiwa juu ya kiasi kipya cha posho na mshahara Zitto alikataa katu katu kuzungumzia hoja hiyo na kusema kuwa mtu wa kuulizwa ni Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Wakati huohuo, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha alisema bado anayo dhamira ya kuwania tena ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.

Masha aliangushwa na mbunge wa sasa jimbo hilo, Ezekia Wenje wa CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2010 na hivyo kupoteza ubunge pamoja na uwaziri.

Masha ambaye alikuwa akihojiwa katika kipindi hicho alisema bado anayo dhamira ya kugombea tena kiti hicho cha ubunge wa Nyamagana lakini hajaamua atafanya hivyo lini.

Alisema kuwa hawezi kutangaza ni lini atafanya hivyo lakini iwapo wananchi wa jimbo hilo watamuhitaji kugombea uchaguzi ujao wa 2015 atafanya hivyo, “Nikigomea tena sitashindwa …suala la kutaka kugombea ni lazima lakini kwa sasa nafanya biashara zangu binafsi…najipanga nitarudi tena katika siasa,” alisema Masha.

EVANS MAGEGE
MTANZANIA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate