Polisi ya Serbia inasema kuwa
kocha wa timu ya Taifa ya Kuwait Goran Tufegdzic ameuawa kwa kupigwa
risasi nchini mwao Serbia na hali yake imesemekana ni mbaya.
Polisi katika mji wa Pozarevac ulio katikati mwa
nchi wamesema kuwa Bw.Tufegdzic alipigwa risasi ya kifua siku ya ijumaa
baada ya ugomvi na jirani juu ya kipande cha ardhi. Baada ya hapo
alimpiga risasi na kukimbizwa hadi hospitali ya mjini Belgrade.
Tufegdzic, ambaye amefanya kazi huko Mashariki
ya kati kwa takriban miaka kumi aliteuliwa kama kocha wa Kuwait mwaka
2009. Aliiwezesha timu hio kufuzu kushiriki kombe la mataifa ya bara
Asia la mwaka 2010 na kuisaidia kushinda kombe la mataifa ya Ghuba la
mwaka 2010.
Mwenyekiti wa chama cha mpira cha Kuwait Sheik
Talal Al-Sabah anasema kuwa amezungumza na mke wa kocha huyo na ana
matumaini atapata nafuu na kwamba familia yake itaweza kupitia kipindi
hiki kigumu''
No comments:
Post a Comment