EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 29, 2012

Maisha ya wasanii Bongo ni maigizo

WENGI wanaamini kuwa maisha ya wasanii wa filamu ni ya kitajiri na kwamba hawana shida kabisa za maisha, hata hivyo ukweli haupo hivyo kabisa.

Maisha yao yamejaaa changamoto nyingi na linapokuja suala la wasanii kuendeleza mwonekano wao mbele ya umma, huwagharimu mno baadhi ya wasanii kiasi cha wengi wao kuishi maisha ya kufoji.

Mwanaspoti limegundua kuhusu maisha hayo ya kuigiza kwa wasanii wengi ambao ni nyota katika tasnia ya filamu za Swahiliwood.

Mara nyingi wasanii hao wamejikuta wakiingia lawama kutoka kwa baadhi ya ndugu zao baada ya kuombwa misaada kwa kuhisiwa wana uwezo.

Wanaposhindwa kutoa misaada hiyo ndipo wanapoingia matatani.

Hivi karibuni mmoja wa wasanii nyota katika tasnia hiyo aliwaambia wanahabari kuwa wasanii wana maisha mabaya kuliko wanavyofikiriwa.

"Jamani msituone hivi, tuna hali mbaya sana. Maisha yetu yamefikia pabaya kwa sababu ya maharamia wa filamu zetu, tunavyoonekana katika filamu si maisha tunayoishi mitaani," alisema.

"Hatuna hizo fedha wanazofikiria watazamaji wetu, narudia tena maisha yetu mabaya sana."

Wasanii wengi wamekuwa wakiishi kwa maisha ya kuigiza kwa kujaribu kujionesha kuwa wana miliki magari ya kifahari wakati ukweli haupo hivyo, japo wengi wanakataa kusema ukweli.

Maisha hayo yanatokana na wasanii kujaribu kujiweka juu kama walivyo wenzao wa nchi nyingine.

NYUMBA
Inasemekana kuwa wasanii wengi katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, wanaishi katika nyumba za kupanga katika hasa maeneo ya Sinza, Tabata, Mwananyamala na Kijitonyama (kwa Dar es Salaam).

Hata wale wanaoishi katika nyumba za familia ni rahisi kukubali hilo iwapo tu nyumba hizo zipo katika maeneo yenye hadhi. 


Lakini ni tofauti na wasanii wanaoigiza vichekesho, kwa mfano wasanii wa Komedi wao wanamiliki nyumba katika sehemu mbalimbali. Masanja, Mac Reagan na Mpoki wao wanamiliki nyumba eneo la Kibada.

Joti anamiliki nyumba yake Ulongoni, Bambo amejenga nyumba Kigogo Mbuyuni, Kingwendu amejenga Mbagala, Mkwere anamiliki nyumba yake Kimara Bonyokwa wakati King Majuto anamiliki nyumba jijini Tanga.

Hawa wote hakuna anayeendesha gari la kifahari hata mmoja, kama yupo basi gari hiyo itakuwa ni Noah.

Pengine linalowafanya wasanii hawa wafanikiwe ni aina ya usanii wao kwani kwao hata daladala wanatumia.

USAFIRI
Katika suala hili, baadhi ya wasanii wamefanikiwa kumiliki magari hata yale ya thamani japo si wote. Lakini wanaonekana kuumia ni akina dada kwani wanalazimka kukodi magari ya gharama kubwa.

Kwa uchunguzi wa Mwanaspoti, gharama hizo zinaanzia Sh300,000 kwa gari kama Hammer au Sh250,000 kwa Range Rover, Vogue au Mercdes Benz. Magari kama Toyota Creaster, Nadia, Luxers na Harrier ni Sh150,000 kwa siku.

Kati ya magari hayo, kuna ambayo wasanii hawa hulazimika kuingia mkataba rasmi kwa ajili ya tahadhari, hii ni kwa mujibu wa mmiliki mmoja wa magari.

Mmiliki huyo anasema kinachowaponza wasanii hao ni kutokuwa na moyo wa subira, kwani kila wakishauriwa kuweka fedha ili kununua magari yao, hawashauriki.
 
Unajua ni kutokuelewa hesabu. Kama mtu ana uwezo wa kunipatia Sh 3 milioni kwa wiki maana yake ana uwezo wa kununua gari. Tatizo hawa jamaa wanapenda maisha ya kubahatisha," alisema.

"Msanii anaweza pia kwenda kwa wakala wa magari na kukopa lake kisha akawa analipa."

Suala la usafiri ndiyo linalowatesa sana wasanii wa kike na wanapokuwa hawana fedha hukodi teksi zenye vioo vya giza ili wasijulikane.

"Hali inapokuwa ngumu hupanda hata bajaj au boda boda (pikipiki) lakini hujifunika baibui," aliongeza.

Hata kwa wale ambao baadhi yao wamekuwa wakitangaza wanamiliki magari, umiliki huo umejaa utata.

Kuna jamaa mmoja inadaiwa alikuwa anawajazia wasanii hao mafuta kwenye magari yao, lakini baada ya kuyumba kiuchumi hata wasanii hao wameyumba katika suala la usafiri.

MAVAZI.
Kwa upande wa mavazi inasemekana kuwa wasanii wengi hukodi kwa ajili ya kurekodia filamu, lakini kiukweli hawana uwezo wa kumiliki nguo za gharama kubwa.

Msanii pekee ambaye ni bingwa wa mavazi ni Patcho Mwamba ambaye inaamika kuwa hata sababu kubwa ya kuingia katika tasnia hiyo ilikuwa ni baadhi ya wasanii kutumia sana nguo zake kwa maana ya kuazima.

MALIPO
Suala la malipo kwa wasanii bado ni kitendawili kwani hakuna malipo rasmi ambayo yanajulikana kwa ajili ya washiriki wa filamu, malipo hutegemea hisani.

Wasanii waliowahi kulipwa vizuri ni Steven Kanumba (marehemu sasa) katika filamu ya Leither Poison, Hamis Kinzasa Twenty Percent katika filamu ya Furaha Iko Wapi.

MONALISA
Yvonne Cherryl 'Monalisa' anasema kuwa hakuna sababu ya kuficha hali halisi ya maisha kwani kwa kufanya hivyo msanii anaweza kukosa watu wa kumsaidia.

"Ni kweli watu wanafoji maisha yao, hawapendi kuonyesha ukweli kuhusu maisha, lakini hilo halipo kwa wasanii wa filamu tu, watu wengi wana tabia hiyo," anasema Monalisa.


ISSA MUSSA
"Sisi wasanii wengi ni waoga wa maisha, tunaigiza hata katika maisha yetu halisi, wasanii wanaosema uongo katika jamii wanafanya hivyo kwa sababu ya kutojipanga na kujaribu kulinda hadhi yao," anasema.

HUSNA POSHI
"Wengi wa wasanii hawana hesabu nzuri za maisha, kuna wanaokodi magari na kusema kuwa ni yao, wanatumia gharama kubwa bila sababu, wanawake hawashauriki na ukimwambia anahisi unamwonea wivu, tunawaacha waishi maisha ya kufoji," alisema msanii huyo anayejulikana kwa jina la Dotnata.

Wasanii hao pia wana sehemu zao wanazopendelea kukutana na kupanga mipango yao, zaidi hukutana Leaders Club, Kinondoni.

Kwa sasa inasemekana kuwa baadhi ya wafanyabiashara kwa upande wa burudani wanawatumia sana wasanii wa filamu katika matamasha mbalimbali kama ni sehemu ya kivutio na si kwa ajili ya kuwawezesha kwa ajili ya kutengeneza fedha.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate