Huu ni ujio mpya wa Fina Mango akiwa katika redi oya Magi FM baada ya kupotea kwenye redio toka wakati akiwa Clouds FM.
Katika kipindi cha Jumamosi, Fina alianza kwa kuichambua sheria mpya ya mafao iliyopigiwa kelele na Watanzania wengi ambapo mwanasheria aliichambua na kuielezea ni kwa nini imepingwa na watu wengi kifungu kwa kifungu.
Baada ya hapo Mheshimiwa Zitto Kabwe aliiongea na Fina huku akijibu maswali mengi sana yaliyotumwa kupitia mitandao ya Twitter, Facebook na Jamii Forums ambayo mengi yalikuwa ya kuhoji kuhusishwa kwake kwenye kashfa ya rushwa, nia yake ya kugombea urais 2015 na uhusiano wake na baadhi ya viongozi ndani ya chama. (Audio ya sehemu hii ya kipindi unaweza kuisikiliza kwa kubofya hapa.)
Wa mwisho kuongea katika kipindi hicho alikuwa Mbunge wa zamani wa Nyamagana, ambaye pia alikuwa Waziri wa mambo ya ndani, Lawrence Masha, ambaye alielezea historia yake ya kisiasa na sababu za yeye kushindwa uchaguzi mwaka 2010 kabla hajapewa nafasi ya kuchagua nyimbo 3 anazozipenda na kujibu maswali ya wasikilizaji.
Wengi walionyesha kufurahia ujio mpya wa Fina Mango, hasa mjadala uliobaki kwenye mitandao ya kijamii baada ya mahojiano na Zitto Kabwe kumalizika.
Shkurani kwa U.F kwa picha na maelezo.
No comments:
Post a Comment