FIDIA KWA WALIOKUWA WAMILIKI WA NYUMBA ZA GEREZANI KOTA AMBAO WAMELAZIMIKA KUHAMA ILI KUPISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MABASI YAENDAYO HARAKA
Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART Agency) uliyoko katika Jengo la Ubungo Plaza Ghorofa ya Kwanza unawakumbusha wote waliokuwa Wamiliki wa nyumba za Gerezani Kota-Kariakoo, wanaostahili kulipwa fidia, wafike katika ofisi hii ili walipwe fidia yao baada ya kukamilisha taratibu za malipo. Ofisi ya Wakala wa Usafiri wa Haraka iko wazi Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.
Watu wote waliokuwa Wamiliki wa nyumba za Gerezani Kota-Kariakoo wachukue barua zao kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gerezani Magharibi, zilizoandikwa tarehe 27 Julai, 2012 zinazoonyesha malipo stahiki ya fidia ya nyumba iliyobomolewa na kama fidia imekwishachukuliwa au bado.
Tafadhali kila aliyekuwa Mmiliki wa nyumba tajwa ambaye hajachukua fidia yake aje na yafuatayo:
Nakala ya mkataba wa umiliki wa nyumba.
Barua yenye picha ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gerezani Magharibi pamoja na barua yetu ya tarehe 27 Julai, 2012.
Jina la Benki na Tawi, Jina la Akaunti na namba ya kuweka fedha za fidia zitakazotolewa.
Kukamilika kwa zoezi hili ni muhimu kwa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka.
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA USAFIRI WA HARAKA
Shukurani kwa taarifa hii: Tina & Ziro blog - ziro99.blogspot.com
No comments:
Post a Comment