MKURUGENZI wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkomo
amewahimiza wasanii na watayarishaji wa filamu Swahiliwood kutumia lugha
ya Kiswahili ikiwa ni katika kulinda na kutukuza Utamaduni wa
Mtanzania, mkurugenzi huyo aliyasema hayo wakati akifungua Semina ya
siku mbili iliyoandaliwa na shirikisho la filamu Tanzania TAFF.
Prof. John Nkomo Mkurugenzi Mamlaka ya mawasiliano (TCRA) aliyewasihi
wasanii kutumia lugha ya Kiswahili na kutangaza utamaduni wetu.
“Nawapongeza kwa kuwa na chombo hiki ambacho lengo lake ni
kuwaunganisha wasanii na kujitafutia maslahi katika utengeneza ji wa
filamu, jambo la kuzingatia ni matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili,
ukiangalia filamu kutoka Bollywood unaona kabisa utamaduni wao, lakini
hata ndugu zetu wanaijeria kupitia filamu zao unaona utamduni wao hadi
sasa hapa nyumbani kuna watu wanaiga wanaijeria katika uongeaji
wao,”alisema Prof. Nkomo.
Simon Mwakifwamba Rais wa TAFF akimkaribisha Prof. John Nkomo kwa ajili ya kufungua Semina ya Mkakati kazi wa TAFF.
Mkurugenzi huyo alisisitiza watayarishaji wa filamu kubaki na
utamaduni wa Kitanzania kwani katika kuiga huko kazi za kitanzania
zimejikuta zikipoteza mvuto kwa kuchanga vitu vinavyojenga maswali
mengi, alisema anaona kasi ya nchi kama Naijeria angependa Tanzania
ifikie huko na hata kuwa nchi ya pili au ya kwanza katika utengenezaji
wa filamu Ulimwenguni.
“Kila jambo ukijipanga linawezekana na kufanikiwa, kwani hata sisi
awali tuliposema tunataka kujenga jengo kubwa ambalo ndilo hili leo
mnafanyia mkutano watu walibeza kwa kusema wataweza lakini leo hii jengo
limekamilika na linatumika,”alisema Prof.
Nkomo.Semina hiyo ya uaandajia wa mkakati kwa ajili mipango ya TAFF
iliandaliwa na shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) na kudhaminiwa na
TCRA semina ilifanyika kwa siku mbili na kuhudhuriwana wadau mbalimbali
pamoja na wawezeshaji kutoka Tanzania Consultech International Limited
mtoa mada alikuwa Prof. Elisante Ole Gabriel mkurugenzi wa maendeleo ya
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
No comments:
Post a Comment