EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 6, 2012

Wanawake 26 wafariki dunia wakijifungua

WANAWAKE 26 wamefariki dunia katika Wilaya ya Manyoni wakati wa kujifungua, huku sababu kubwa ikitajwa ni utumiaji dawa za kienyeji.

Wanawake hao walifariki dunia kipindi cha mwaka 2010/2011, eneo la Itigi likitajwa kuongoza kwa utumiaji dawa za kienyeji kwa lengo la kuharakisha kuzaa.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya ya Manyoni, Grace Mwegoha alipozungumzia utekelezaji wa Mradi wa Ushiriki Sawa kwa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Jinsia (TMEP).

“Wanadanganyana sana, utakuta mama ameanza kuumwa uchugu anapewa dawa za kienyeji ili azae haraka hatimaye anakufa na mimba,”alisema Mwegoha na kuongeza:
“Itigi ndiyo wanaongoza, lakini tunajaribu kuwaelimisha na tukiwakamata tunawarudisha nyumbani.”
 
Mwegoha alisema kati ya vifo 14 vilivyotokea mwaka 2010, vitano vilisababsihwa na utumiaji dawa za kienyeji, mwaka jana vifo vya wazazi vilikuwa 12 na viwili vilisababishwa na matumizi ya dawa za kienyeji.
Alisema vifo vingine vilisababishwa na kifafa cha mimba, kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, uambukizo baada ya kujifungua, malaria, upungufu wa damu, ugonjwa wa Ukimwi, maji kuingia kwenye mishipa ya damu na matatizo ya moyo.

Hata hivyo, Mwegoha alisema vifo hivyo havitabiriki kwani wakati mwingine vinapanda na kupungua.
Mratibu huyo alisema wanatarajia vifo hivyo vitapungua hasa baada ya ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi, kwasababu wanawake wengi walikuwa wanakosa matunzo mazuri kutoka kwa waume zao.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dk Antipas Swai alisema mradi huo umewasaidia kwasababu kazi zao nyingi zinahitaji uhamasishaji na kuelimisha wananchi, ili waelewe masuala mbalimnbali ya afya ya uzazi hasa kumhusisha mwanaume.

“Kwenye kliniki zetu maelekezo mengi yalikuwa yanatolewa kwa wanawake, lakini tuliona mengi yalikuwa hayafiki kwa wanaume,”alisema Dk Swai.
Alisema changamoto iliyopo ni kuweka mazingira ya kumfanya baba akienda kliniki aweze kushiriki vizuri, ili wanawake waone kama suala hilo ni jambo la kawaida.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate