EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 28, 2012

AIRTEL YAZINDUA MINARA INAYOTUMIA SOLAR VIJIJINI

Picha ya chini wa kwanza ni injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege akitoa ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano uliowekwa na Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano katika kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia nguvu za  Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw Jackson Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda mtambo mpya wa mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili kufikisha  huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bw, Beda Kinunda na kushoto ni Injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi ilifanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.

Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda Meneja wa  Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa Airtel unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar)  wakizungumza  na Mwenyekiti  wa kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu (shoto) mara baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano unaotumia nguvu za Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani, Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya jua kwa lengo la kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo bado hakujafikiwa na umeme wa taifa.
Kulia ni Injinia wa airtel mkoani Iringa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu anaedadisi ili kupata ufafanuzi wa jinsi mnara wa Airtel unaotumia Nishati ya jua (solar) unavyofanya kazi mara baada ya Airtel kuzindua mnara huo kijijini hapo jana.

 Taarifa kwa vyombo vya habari
Airtel yazindua Minara ya Mawasiliano inayotumia umeme wa Jua
. kupunguza changamoto za umeme vijijini
. kurahisisha mawasiliano madhubuti
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia  Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa.  Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake nchini.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.

“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwana Mpululu.
Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”

Kampuni ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa iringa Iringa vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana na ina vijiji na miji 50.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate