Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kupitia CCM (katikati) akiwa na Naibu Meya John Minja (CCM) wakitambulishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe baada ya kutangazwa washindi kufuatia uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.
HATIMAYE Halmashauri ya jiji la Mwanza imerudi chini ya uongozi wa CCM baada ya kushinda nafasi ya Umeya na Unaibu meya katika uchaguzi uliofanyika jana kufuatia kugawanywa na kuwa halmashauri mbili huku uchaguzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela ukiahirishwa baada diwani wa CHADEMA aliyevuliwa uanachama na kamati kuu, Henry Matata kuweka pingamizi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji, Msimamizi wa uchaguzi, Wilson Kabwe alisema mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula alishinda nafasi ya umeya baada ya kupata kura 11 na kumshinda upinzani wake kutoka Chadema Charles Chinchibera ambaye alipata kura nane. Nafasi ya unaibu meya ilichukuliwa na diwani wa kata ya Igogo, John Minja ambaye alipata kura 10 na kumbwaga mpinzani wake Diwani kata ya Mirongo (CUF), Daud Mkama aliyepata kura nane.
Katika uchaguzi huo CHADEMA iliingia mkataba na CUF na kuachiana nafasi ya Unaibu Meya ambao walishindwa kuipata. Kabla ya uchaguzi huo kuanza majira ya saa saa 4 asubuhi, katika eneo la Ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza kulionekana kuwepo kwa ulinzi mkali wa askari wa kutuliza ghasia (FFU) huku barabara ya kuelekea katika Hospitali ya mkoa ya Sekou Toure ikiwa imefungwa. Walioruhusiwa kupita katika barabara hiyo walikuwa ni madiwani, watumishi wa halmashauri ya jiji la Mwanza na waandishi wa habari, huku wengine wakitakiwa kuzunguka.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa Nyamagana, Katibu wa Itikadi, siasa na Uenezi wa CCM, Nape Mnauye alisema CHADEMA wamevuna walichopanda kwa ubabe wao, “Hizi ni salamu kwa wana CHADEMA, Dkt. Slaa alikuwepo hapa Mwanza alipoona upepo mbaya jana (Juzi) usiku, ubabe wao umewafikisha hapo walipo,” alisema Nape na kuongeza CCM bado ipo imara tofauti na Dkt. Slaa anavyoona. Alisema madiwani wameamua kuirudisha CCM kuliongoza jiji la Mwanza hivyo kuwaomba washirikiane katika kuliletea jiji maendeleo kwa kuanza kukabiliana na changamoto ya migogoro ya ardhi.

No comments:
Post a Comment