EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 27, 2012

HAKIELIMU WAZINDUA MATANGAZO KUHAMASISHA ELIMU YA AWALI

Baadhi ya walimu na wafanyakazi wakionesha mabango kuelezea maboresho ya elimu ya awali katika uzinduzi wa matangazo mapya ya HakiElimu juu ya kampeni za maboresho ya elimu ya awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia, akisoma taarifa kuzindua kampeni hizo. Kushoto ni Arcard Rutajwaha kutoka TECDEN na kulia ni Bi. Mary Kabati kutoka TAHEA.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Awali ya Mchangani iliyopo jijini Dar es Salaam wakionesha bango lenye ujumbe juu ya maboresho ya elimu ya awali.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia, akigawa zawadi ya vifaa anuai vya masomo kwa wanafunzi wa shule ya awali ya Mchangani mara baada ya uzinduzi huo.
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
TAASISI ya HakiElimu imezindua matangazo mapya ya redio na televisheni ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha jamii na Serikali juu ya umuhimu wa elimu ya awali kwa watoto kabla ya kujiunga na darasa la kwanza.
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za HakiElimu na kuhudhuriwa na baadhi ya walimu na wanafunzi wa awali, waandishi wa habari, wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, pamoja na malezi na makuzi ya watoto.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia alisema shirika hilo lemeamua kuzindua kampeni hiyo iliyopewa jina la “Boresha Elimu ya Chekechea” lengo kuu likiwa ni kuitaka Serikali itimize ahadi na wajibu wake wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wote wa elimu ya awali.

Mkurugenzi huyo alisema elimu ya awali kwa mtoto ni muhimu sana katika kujenga msingi imara kielimu na endapo elimu hiyo itatolewa kikamilifu, inakuwa ni msingi imara kwa mtoto katika elimu yake ya baadae na pia elimu hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili.
“Katika Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha umuhimu wa elimu ya awali, inapotamka; ‘Tafiti kadhaa zilizofanyika nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza. Kutokana na kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu na kila shule ya msingi inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali’,” alisema Missokia.
Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni hii HakiElimu imefanya tafiti katika sehemu mbalimbali nchini na kubaini hali ya utoaji wa elimu ya awali na mazingira yake inatia huruma kwani elimu hiyo inavyotolewa katika mazingira yasiyofaa jambo ambalo linachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

“Kama ilivyo katika elimu ya msingi na ile ya sekondari, elimu ya awali imegubikwa na changamoto nyingi. Baadhi ya changamoto hizi ni  upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, unaosababisha mrundikano mkubwa katika madarasa, ukosefu mkubwa wa walimu wenye taaluma ya elimu ya awali pamoja na vifaa vya kufundishia. Aidha, kutokuwepo na tofauti ya kimadarasa katika elimu ya awali (yaani watoto wa umri wa miaka 5 na miaka 6 kusoma katika darasa moja), na wingi wa masomo pia ni changamoto,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa licha ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, katika makadirio na matumizi ya wizara yake ya mwaka 2012/13, kukiri kuwa Serikali imetoa mwongozo kwa kila shule ya Msingi kuwa na darasa la Elimu ya Awali, lenye madawati yanayolingana na hali ya watoto wa elimu hiyo, kujenga vyoo kwa ajili ya watoto wa Elimu ya Awali wasiingiliane na wale wa shule za msingi, lakini bado kuna mapungufu makubwa katika utekelezaji wake.

"Baada ya kuona madhara ya kukosa elimu bora ya awali kwa watoto wetu, HakiElimu inatoa wito kwa watanzania wote nchini wenye mapenzi mema na maendeleo ya taifa letu kuungana nasi katika kampeni hii kwa njia zifuatazo; Kuhimiza wananchi wote wenye watoto wenye umri wa kuandikishwa shule za awali wafanye hivyo kwa wingi. Kuna baadhi ya sehemu inaripotiwa wazazi bado hawajaelewa umuhimu wa kuwapeleka watoto katika madarasa haya ya awali.
"Kuwabana viongozi wetu tuliowachagua kuanzia mwenyekiti wa mtaa, diwani na Wabunge wetuwanachukua hatua kukabiliana na changamoto zilizopo ili kufanikisha Elimu bora ya Awali kwa watoto wetu.

Wananchi kuandika barua kwenye magazeti mbalimbali hapa nchini zikielezea hali ya elimu ya awali inavyotolewa katika maeneo mliyopo."
HakiElimu imeshauri barua zinazoandaliwa na wananchi kuzituma moja kwa moja kwa Wahariri wa magazeti wanayoyasoma kupitia anuani zilizopo katika gazeti husika, au wanaweza kuzituma kupitia sanduku la barua 79401 Dar es Salaam zikiwa na kichwa cha habari ‘BORESHA CHEKECHEA’, ambapo HakiElimu itafanya kazi ya kuzipeleka katika magazeti mbalimbali nchini.
Aidha, ili kuchagiza mafanikio katika sekta ya elimu, HakiElimu imeandaa vipindi vya radio katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Tabora, Tanga, Kagera, Dodoma na Mara ambavyo vitatoa nafasi ya Marafiki wa Elimu kujadili jinsi gani elimu ya awali inaweza kuboreshwa.
Hata hivyo kwa Watanzania wanaotumia mtandao wa 'Internet' wanaweza kushiriki kampeni hii kwa kutembelea;www.facebook.com/hakielimuwww.twitter.com/hakielimuwww.hakielimu.blogspot.com na kuangalia matangazo mapya waweza kutembelea YouTube kupitia www.youtube.com/hakielimutz.

* Habari hii imeandaliwa na mtandao wa www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate