Na Sifael Paul
Mume wa Miss Tanzania 2004, Faraja Kota ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (pichani) amefanyiziwa mtandaoni baada ya watu (wadukuzi) kuingilia akaunti yake ya barua pepe (e-mail) na kuanza kuwasiliana na watu wake wa karibu wakiwapiga mizinga ya fedha.
Waziri huyo wa Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini, alikutwa na mkasa huo hivi karibuni ambapo aliandika kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter kuwa watu wake wa karibu wawe makini na waleti zao kwani siyo yeye anayewasiliana nao kwa njia ya barua pepe bali ni hao waliomfanyia kitendo hicho.
“Kuna baadhi ya watu walidukuzi (hacked) akaunti yangu ya barua pepe, wapo bize wanachukua fedha kwa watu kwa kutumia jina langu. Tafadhali chungeni waleti zenu. Inasikitisha!,” aliandika Waziri Nyalandu.
Mchezo huo umekuwa ukifanywa sana na wadukuzi hasa kwa watu wenye majina makubwa wakiwemo wanasiasa na wasanii hivyo jamii inapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanapopigwa mizinga wafanye mawasiliano kabla ya kutuma fedha kwa mtu husika.
No comments:
Post a Comment