EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 28, 2012

Zitto: Ubunge sasa basi badala yake anajipanga kuwania urais 2015

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao. 
“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.endelea kupitia audifacejackson blogspot..“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

 “Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.

 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

 “CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.Chanzo cha habari ni Gazeti la Mwananchi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate