HII NDIO KAULI YA WEMA...soma hapa ndo mastaa wetu
Diamond Platinums akiwa katulizwa pajani mwa Nuzlah Abubakary
Mnatuonaaa
Mtoto wa Kiislam haswaa.
Nani amenuuna.
Shemeji yetu mpya Nuzlah huyo kapooz.
Baada ya maneno ya hapa na pale.Mara karudiana na Wema ,mara bado yuko na Jokate nk.Atimae Msanii HoT anashika usukani kila idara kwenye game ya Bongo fleva kwa sasa Diamond Platnums,ameamua kumuweka wazi mpenzi wake mpya anaejulikana kwa jina Nuzlah Abubakar.Diamond ambae bado hajaoge chochote zaidi ya kuweka picha hizo kupitia mtandao wake wa facebook na twitter kua yuko engaged na mrembo huyo,amewaacha mashabiki na watanzania waliowengi wakijiuliza wenyewe pasi nakupata majibu yoyote toka kwa wahusika.
Nuzlah ambae nae kwa upande wake pia anasomeka kua yuko engaged kwa Mtoto huyo wa kimanyema Diamond.Nimfanyakazi wa shirika la umoja wa mataifa(United Nations) as Administrative assistant, anaeishi nchini Kenya kwa Raisi Mwaikibaki.kama anavosomeka kwenye profile yake kwenye mtandao wa facebook.Hivyo isije kua ajabu kumuona Mnyaama Platnumz kwenda kwa kina Prezoo au kuamia uko mazima kama ilivyo kwa wasanii wengine kama AY,Hussein Machozi na RayC.
Habari hii itawafanya walewaliokua na shauku ya kujua kati ya Wema na Jokate ni nani basi anashikilia nafasi yake kwa Diamond.Jibu ni kwamba wote Imekula kwao kwani Raisi uyo wa wasafi sasa ametulia kwa mtoto wa Kislam shombeshombe saafi.Bilashaka safari ya Diamond kuingiza jiko Mjengoni inakaribia soon.
Nahichi ndicho alichosema WEMA Baada ya taarifa hizi
"KUNA JINI KISIRANI KAIINGIA KWENYE UTAMU WA PENZI LANGU....."
Kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa facebook .
Watu kibaao wamecoment wanayojua wapo waliompa pole ,kumponda ili mladi tafrani .Ndo mastaa wetu lakini.
Zilipendwa Jokate
Zilipendwa Wema.
Ukitaka jua mengi zaidi na wawili hawa wanasemaje endelea kupitapita apa.ntakuletea Xclusive za kutosha.
No comments:
Post a Comment