
Mabadiliko hayo ya jina la uwanja wa ndege ni sehemu ya utangazaji na mkakati wa kukuza utalii kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ni rahisi watalii kufika katika mbuga ya wanyama ya Sengereti wakitokea Mwanza.Kauli ya kuridhia mabadiliko hayo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo wakati wa ufunguzi wa wiki ya Utalii kitaifa inayoendelea jijini hapa baada ya Mwenyekiti wa Chama wa Watalii Mwanza (MTA) kutoa pendekezo lililoungwa mkono na wakuu wa mikoa ya Geita na Simiyu.
Ndikilo alisema serikali inaendelea na juhudi za kuweka miundombinu muhimu kwa maendeleo ya sekta ya utalii hapa nchini ambapo ujenzi na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mwanza kitakuwa na hadhi ya kimataifa.Alisema uwanja huo utakapokamilika utapewa jana la ‘Serengeti international Airport’ kama ilivyopendekezwa.
No comments:
Post a Comment