EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 24, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI(CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIKA kusimamia uongozi unaozingatia misingi muhimu ya haki za binadamu, sheria na utawala bora, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza msimamo wake wa kutotoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel ten, Daudi Mwangosi, kilichotokea Septemba 2, 2012, Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.
Msisitizo huo umekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo kukiandikia barua (isiyokuwa na Kumbukumbu Namba) CHADEMA, akiomba kamati yake ikutane na viongozi wa chama Septemba 25, ili kutafakari tukio hilo na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kutokea hapa nchini.
Itakumbukwa kuwa Marehemu Mwangosi aliuwawa na Jeshi la Polisi akiwajibika kwa jamii katika shughuli za uandishi wa habari, wakati askari wa jeshi hilo walipovamia ofisi za CHADEMA Kata ya Nyololo na kuanzisha vurugu wakati wanachama walipokuwa wakiendelea na shughuli halali za ndani za chama.

Katika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CHADEMA kimesema wazi kuwa hakiko tayari kukaa na kutafakari juu ya kifo cha Mwangosi kama ilivyopendekezwa na kamati hiyo, kwani haipo kwa mujibu wa sheria, huku pia ikiwa imeundwa na mtu ambaye kanuni za msingi za utawala bora, zinamtaka awe amejiuzulu au kufukuzwa kazi, kupisha uchunguzi huru juu ya mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la polisi, linalowajibika kwake kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Kamati hiyo pia inawahusisha polisi ambao katika tukio hilo ni watuhumiwa namba moja.Mbali ya kusisitiza kuwa haiwezi kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haipo kwa mujibu wa sheria, CHADEMA kimeshangazwa na kusudio hilo la Kamati ya Nchimbi kutoa mwaliko wa kutaka kukutana na viongozi wa CHADEMA, huku ikitambua wazi msimamo wa chama hiki juu ya uwepo wa kamati hiyo mara tu ilipoundwa.


Kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haina mamlaka ya kisheria ya kuhakikisha ukweli mtupu unajulikana na haki ionekane ikitendeka kutokana na kifo hicho na vingine vingi ambavyo vimefanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, ni kuhalalisha uvunjivu wa haki za binadamu, Katiba na sheria za nchi. CHADEMA haiko tayari kuona hali hiyo ikifanyika.Katika kuonesha msisitizo wa kutokubali mwaliko wa Kamati ya Nchimbi inayotaka kutafakari matukio ya vifo ambapo Jeshi la Polisi limewanyang’anya watu wasio na hatia haki ya kuishi, katika barua yake ya majibu, CHADEMA pia kimeambatanisha nakala ya barua ya tarehe 10/09/2012 iliyowasilishwa kwa Rais, ili kamati hiyo iweze kuelewa msimamo mpana wa chama kuhusu mauaji ya kisiasa yanayofanyika nchini.


Kwa taarifa hii, CHADEMA kinaendelea kusisitiza maazimio ya Kamati Kuu ya Chama, ambayo pamoja na mambo mengine, iliazimia kuwa kutokana na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kisiasa yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli halali za chama, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu au Rais awawajibishe kwa kuwafukuza kazi ili wapishe uchunguzi huru na wa haki.

Pia Kamanda wa Polisi Iringa, Michael Kamuhanda, Kamanda wa FFU Mkoa wa Morogoro, na askari wote wanaoonekana kwenye picha wakiwa wamemzunguka Mwangosi muda mfupi kabla hajalipuliwa na kuuwawa, wakamatwe haraka na kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Mwangosi. Kinyume na hapo ni kuchezea akili za wapenda haki na uwajibikaji, ikiwa moja ya misingi ya amani Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.


CHADEMA inapenda kusisitiza kuwa itatoa ushirikiano kwa chombo kitachoundwa kwa mujibu wa Sheria huku ikitilia msisitizo wito kwa Rais kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji kuchunguza vifo vyote vyenye utata na vinavyohusishwa na masuala ya kisiasa kama tulivyopendekeza kwake hapo kabla.

Imetolewa leo Septemba 24, 2012 Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Ofisa Habari wa CHADEMA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate