Kocha mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Upande wa Yanga, uliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ambaye alishuhudiwa na viongozi wengine wa klabu hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako na Majjid Suleiman, mmoja wa watu muhimu kwenye klabu hiyo. Habari inakuja...
|
Brandts kulia na Sanga kushoto |
|
Anamwaga wino |
|
Brandts kulia na Sanga kushoto |
|
Brandts na Sanga |
|
Brandts na Sanga
KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesema kwamba atajitahidi kadiri ya uwezo wake, kuhakikisha anaiongoza timu hiyo kushinda mechi ya Jumatano dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC ingawa anajua utakuwa mtihani mgumu.
Brandts alisema hayo, baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam asubuhi hii.
Alisema kwanza anaushukuru uongozi wa klabu hiyo kuwa kumuamini, na anaafiki kwa kiasi kikubwa kupewa nafasi ya kurithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, aliyetupiwa virago wiki iliyopita, baada ya kuitumikia Yanga kwa siku 80.
“Muhimu kwangu, nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuipa matokeo mazuri klabu kwa asilimia mia moja. Nilikuwa Uholanzi, nikapigiwa simu na Mwenyekiti, Yussuf Manji, akaniambia anataka nije kufanya kazi Yanga, nilikuwa nina ofa nyingi, ila nilivutiwa naye (Manji), aliponiambia falsafa na sera za klabu, anataka kuindeleza klabu.
Kitu kingine ni kuhusu timu, kama kocha, kweli tuntaka kushinda kila mechi, lakini tunataka kucheza soka ya kuvutia. Jambo muhimu kwangu ni kufanya kila mchezaji mmoja mmoja acheze vizuri, na timu icheze vizuri, kwa sababu hakuna bora zaidi ya timu,”alisema.
Brandts pia alizungumzia nihdamu, akisema; “Kuzingatia nidhamu, ni muhimu si hapa tu Afrika, hata Asia na Ulaya kwa sababu, ukitaka kuamka saa moja kamili amka saa moja kamili na ukitaka kujenga timu nzuri, muhimu kujituma, hata mimi nilipokuwa nacheza ilikuwa hivyo pia, ni muhimu kujivunia timu unayochezea na kila mchezaji anatakiwa kujivunia kuchezea Yanga,”alisema.
Kuhusu kazi, alisema; “Kitu kingine, kuna mechi kesho na kuna mechi Jumatano, dhidi ya Simba itakuwa ngumu sana, tutafanya kila tunachoweza kuhakikisha tunashinda, naijua Yanga nimekuja hapa miaka miwili, ni timu nzuri. Sasa nakwenda kujaribu kuboresha timu, najiona mwenye bahati kusaini mkataba na timu hii,”alisema.
Brandts alikuja mwaka jana na mwaka huu kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, akiwa na APR ya Rwanda na mara zote, Yanga iliibuka bingwa, mwaka jana ikifundishwa na Mganda Sam Timbe na mwaka huu ikifundishwa na Mbelgiji, Saintfiet.
Via BIN ZUBEIRY
|
No comments:
Post a Comment