SIKU chache baada ya madai ya kuipindua ndoa ya Shufaa, Miss Ruvuma 2008, Isabella Mpanda ‘Bella’ amemfumania mchumba’ke, Karama Bakari ‘Luteni Kalama’ akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Faidha Omar ‘Sister Fay’.
Erick Evarist na Gladness Mallya
Shufaa na Kalama walikuwa mke na mume kabla ya mapinduzi aliyoyafanya Bella hivi karibuni.
Kwa mujibu wa chanzo, ishu hiyo ilijiri juzikati ambapo Bella alimfumania mpenzi wake huyo wakati akiwa amekwenda kumtembelea nyumbani kwake, Tabata Segerea, Dar.
“Isabella alikuja kumtembelea Kalama, akanasa meseji za mapenzi kwenye simu yake zikitoka kwa Sister Fay,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Meseji zenyewe zilikuwa zikimtaka Kalama amfuate demu huyo kwenye Baa ya Rose Hill ya kulekule Segerea, ndipo alipomuandalia mtego kabambe wa kwenda kumfumania.”
Imeelezwa kuwa, Kalama bila kujua kama Bella aliziona meseji hizo, alisingizia kupata dharura kwamba alitakiwa kufika studio kurekodi wimbo ambapo Bella alimruhusu kwani tayari alishajua kinachoendelea.
Baada ya Kalama kutoka, Bella akafuatia kwa nyuma hadi eneo la tukio huku akiwa amevalia vazi lililoziba sura yake.
Alizunguka nyuma ya baa hiyo na kuwakuta wawili hao wakijiachia huku Sister Fay akimnywesha bia Kalama bila kujali mazingira ya wazi.
Muvi la kivita lilianzia hapo, Bella alimvaa Sister Fay na kumkandamiza magumi mfululizo huku ‘mwizi’ huyo akijibu mashambulizi dhaifu.
“Kalama alipoona soo limekuwa kubwa, watu wanaanza kujaa alitimua mbio ndefu,” kilisema chanzo.
Hata hivyo, habari zinadai baadhi ya watu waliokuwepo kwenye eneo la tukio waliamua ugomvi huo huku Bella akitoa vitisho kwa mwizi wake kuwa atahakikisha anamuonesha kama yeye ni mtoto wa mjini.
No comments:
Post a Comment