Hatimaye Bosi wa Chelsea, Roberto di Mateo (42) ametimuliwa klabuni hapo kufuatia matokeo mabaya ya hivi karibuni.
Kushindwa
3-0 katika katika mechi ya kufa na kupona jana dhidi ya Juventus ya
Italia kumechangia sana kumfanya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kupoteza uvumilivu kwa Di Mateo.
Taarifa
ya klabu ilisema: "Matokeo ya hivi karibuni yamekuwa mabaya, mmiliki na
bodi imeona hakuna njia nyingine zaidi ya kufanya mabadiliko.

"Klabu
inakabiliwa na kazi ngumu mbele katika kufuzu kwa hatua Knockout ya
Ligi ya Mabingwa pamoja na kudumisha changamoto kali kwa ajili ya juu ya
Ligi Kuu.
"Lengo letu ni kubaki katika ushindani kadri iwezekanavyo katika nyanja zote.
"Mmiliki na bodi tunapenda kuwashukuru kwa yote ambayo Roberto amefanya kwa klabu tangu alipoichukua rasmi mwezi Machi.
"Roberto alisaidia kutuongoza sisi kihistoria na kupata ushindi wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la saba la FA.
"Sisi kamwe hatuwezi kusahau mchango mkubwa alioufanya katika historia ya klabu yetu na daima anakaribishwa muda wowote Stamford Bridge.
"Klabu itatangaza muda mfupi ujao kuhusu nani atakuwa kocha mpya."
Mtu ambaye anatajwa sana kuchukua nafasi ya Di Mateo ni kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez kama kocha wa muda huku Chelsea ikiendelea kumuandaa Pep Guardiola kuwa kocha wa kudumu hapo baadae.

Via saluti5

No comments:
Post a Comment