Ni wazi kuwa Kocha Roberto Di Matteo lazima afukuzwe Chelsea - ni suala la lini lifanyike jambo hilo.Inaaminika tayari Chelsea wanakaribia kumalizana na kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez kama suluhisho la muda.

Suala la kumuacha nje Fernando Torres nalo limemgharibu Di Mateo kwa mechi ya jana usiku kujenga au kubomoa dhidi ya Juventus. Chelsea ikachapwa 3-0.
Na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ataongeza jitihada zake ya kumnasa bosi wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola huku timu yake ikikabiliwa na tishio la kutolewa mapema mapema kwenye Ligi ya Mabingwa.
Di Matteo amekubali kubeba lawama zote kwa kipigo cha jana.
Akasema: "Mimi nina wajibika kwa matokeo haya, lawama zote ni za kwangu.
"Ni jioni hasi kwa ajili yetu na kama kuna mtu wa kubebeshwa lawama, basi ni mimi.
"Ni
Mimi niliyechagua timu nilishawishika kuamini kuwa ilikuwa timu sahihi
ya kushinda dhidi ya Juventus, au angalau kupata sare. Hivyo lawama ni
zangu. "
Di Matteo anajua anaweza kutimuliwa wakati wowote licha ya kuipa taji la Ulaya klabu hiyo miezi sita iliyopita.
Aliongeza: "Sikuzungumza na mtendaji yeyote kwa yoyote usiku wa leo na mimi pengine si mtu sahihi kuuliza juu ya hatma yangu.
"Kwa sasa niko hapa Chelsea na nadhani nitakuwa hapa kwa siku zijazo.
"Kimahesabu,
bado inawezekana kuhitimu raundi ya pili. Nani anasema kwamba Juventus
si kwenda kupoteza kwa Shakhtar katika mchezo wao wa mwisho?
"Sisi
tunachotakiwa ni kuhakikisha kuwa tunashinda mchezo wetu wa mwisho na
ni matumaini yangu kuwa pointi 10 zitatosha kutuvusha.
"Tuna
tunauchukulia kwa uzito mchezo mwingine mkubwa dhidi ya Manchester City
siku ya Jumapili katika ligi kuu ya Uingereza. lakini wakati matokeo
yanapokuwa mabaya ni kila ulichofanya kitahojiwa.
"Katika klabu kubwa kama hii, unapopata
hata matokeo mabaya machache, ni lazima utakuwa chini ya shinikizo, nah
ii ni tangu siku ya kwanza na ndivyo inavyoendela "Via Saluti5 (www.saluti5.com)
No comments:
Post a Comment