CHAMA cha Washereheshaji Nchini (Sherehe Arts Association –SAA),
kinatoa pole za rambirambi kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,
familia ya Marehemu Hussein Ramadhan
‘Sharomilionea’ kutokana na kifo
cha msanii huyo.
Rambirambi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, MC Bryceson
Makena, alipokuwa akizungumza na mwanadishi wa habari hizi.
Alisema SAA inawatakia wanafamilia wote ujasiri wa kulipokea jambo
hilo na kuvuta subira kwani wote njia ni moja ila wakati ndio tofauti.Pia ametoa wito kwa wasanii wote nchini kuwa na umoja na mshikamano endelevu katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment