EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, November 1, 2012

HAYA NDO MAJINA YA WATOTO WA VIGOGO WALIOJAZANA "IDARA YA AFYA" NA "BoT".... HUU NI UPENDELEO NA UONEVU MKUBWA.

                       Habari hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la Jamhuri.
Siku chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, JAMHURI imebaini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo, wametoa waraka wakihoji namna watoto hao wa vigogo walivyoweza kushika nyadhifa kubwa katika manispaa hizo, ilhali watumishi wengine wenye sifa, ama wakiachwa au wakipelekwa mbali na Jiji la Dar es Salaam.Katika waraka huo, ambao JAMHURI imepata nakala yake, wanatajwa baadhi ya watoto wa vigogo na nyadhifa zao kuwa ni Janeth George Kahama, ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji. 



Huyu anatoka katika familia ya Mzee George Kahama, mmoja wa mawaziri wawili walio hai wa kwanza katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika huru. Mwingine aliye hai ni Job Lusinde.Waraka huo pia unasema nafasi ya Mganga Mkuu Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam inashikwa na Dkt. Hawa Rashidi Kawawa. Huyu ni mtoto wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanganyika, Waziri Mkuu wa Tanzania, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).“Hivi ni kweli watoto hawa wa wakubwa ndiyo wenye sifa tu za kushika nyadhifa hizi? Kweli, wanaweza kuwa na sifa, lakini iweje wasipelekwe Tandahimba, Kibondo au Karagwe? Kwanini Dar es Salaam tu?” Wamehoji waandishi wa waraka huo.



Wameendelea kusema kuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ni Dkt. Gunini Kate Kamba.  Huyu ni mtoto wa Kamba aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na ndani ya CCM. Wadhifa wa karibuni kabisa aliokuwa nao ni wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki.Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo ni Dkt. Asha Omar Mahita. Dkt. Asha ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omar Mahita.Mtoto mwingine wa kigogo ni Dkt. Amani Kighoma Malima ambaye ni Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Temeke. Huyu ni ndugu yake na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.Dkt. Amani ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini. Mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti alikuwa Waziri wa Fedha.Aidha, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, ingawa si mmoja wa watoto wa vigogo, lakini alikuwa na uhusiano wa karibu mno wa kikazi na aliyekuwa Mganga Watoto wengine wa vigogo waliojazwa Idara ya Afya.Watoto wa vigogo wameshika nafasi zote za Jiji - Ilala, Temeke, KinondoniMkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa; aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka huu kutokana na shinikizo la madaktari waliogoma.

“Haya ni majina ya baadhi tu ya watoto wa vigogo katika Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake. Tunauliza, iweje watoto wa wakubwa tu ndiyo washike nyadhifa hizi kwa Dar es Salaam na si mikoani?”Umehoji waraka huo.

Wiki iliyopita, JAMHURI iliandika taarifa ya kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya BoT. 

 -----------------------------------------------------------
Hadi sasa, majina yanayovuma ya watoto hao ni: 
1. Pamela Edward Lowassa, 

2. Filbert Tluway Sumaye,
 3. Zaria Rashidi Kawawa,
 4. Harriet Matern Lumbanga, 
5. Salama Ali Hassan Mwinyi,
 6. Rachel Muganda, 
7. Salma Omar Mahita, 
8. Justina Joseph Mungai, 
9. Kenneth Nchimbi, 
10. Blasia William Mkapa, 
11. Violet Philemon Luhanjo, 
12. Liku Kate Kamba, 
13. Thomas Mongella na 

14. Jabir Abdallah Kigoda.
------------------------------------------------------------------
Kuwapo kwa watoto wa wakubwa katika sehemu nyeti na nzuri kumeanza kuzua minong’ono ya upendeleo miongoni mwa wananchi.Mmoja wa wananchi amehoji hali hiyo kwa kusema,“Ninachojiuliza na sipati majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea coincidence (bila kutarajia) BoT ikaajiri watoto 14 wa vigogo; je, coincidence hiyo hiyo inaweza kutokea kwenye Wizara ya Elimu watoto wenye majina kama hayo hayo wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini, ambako hakuna maji wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila kujali kuwa mishahara imechelewa na hawajapandishwa vyeo; na wakati huo huo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?“Hivi kweli binadamu wote ni sawa kwa maana ya fursa za ajira bila kuangaliana usoni, hasa BoT?

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate