HALI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imezidi kuwa tete baada ya kuwapo mpango wa kutaka kufuta matokeo ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kwa madai kuwa uchaguzi wake ulitawaliwa na rushwa kupita kiasi.
Mbali ya matokeo ya UVCCM, duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa chama hicho pia kimepanga kufuta matokeo ya uchaguzi katika baadhi ya maeneo yaliyolalamikiwa kwa vitendo vya rushwa.
Wilaya ya Hanang ambako kulikuwa na mnyukano mkali kati ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, inaelezwa kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Dk. Nagu, yanaweza kufutwa.Sumaye ndiye kada wa kwanza wa CCM aliyejitokeza hadharani kulalamikia matumizi ya rushwa ya mtandao kwenye uchaguzi huo ambapo aliangukia pua.
Mkakati wa kutaka kufuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM, unadaiwa kusukwa na mtoto wa kigogo wa chama hicho taifa.Kwa mujibu wa habari hizo, mtoto huyo alimpigia simu mmoja wa wagombea walioshindwa katika nafasi ya mwenyekiti kutoka Zanzibar na kumtaka aje jijini Dar es Salaam kwani Rais Jakaya Kikwete alitaka kuonana naye.
Baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, kijana huyo alifikia katika Hoteli ya Bondeni na alipotaka kuonana na Rais Kikwete, aliambiwa yupo ziarani mkoani Kilimanjaro na kwamba amemwachia maagizo.Kwa mujibu wa habari hizo, maagizo yanayodaiwa kutoka kwa Rais Kikwete ni kumtaka kijana huyo kuandika barua ya malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa UVCCM ili kuwa na msingi wa hoja ya kutaka kufuta matokeo hayo.
Habari zinaeleza kuwa, kijana huyo aliandika barua hiyo ya malalamiko na kueleza sababu kubwa tatu za kutaka matokeo ya uchaguzi huo yafutwe.
Sababu hizo ni pamoja na kukithiri kwa vitendo vya rushwa ya mtandao, matumizi mabaya ya madaraka ambapo Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, anadaiwa kutumia nafasi yake vibaya kumsaidia mgombea ashinde.
Habari zinasema kuwa tayari barua hiyo imewasilishwa kwenye sekretarieti ya CCM kwa ajili ya uamuzi.Ukiachia mkakati huo wa kumtumia rais kutaka kufuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM, mkakati mwingine unasukwa na baadhi ya vigogo wa chama hicho ili kuionyesha jamii kwamba CCM imekerwa na rushwa.Mmoja kati ya vigogo wa chama hicho tawala, aliliambia gazeti hili kwamba ili kurejesha heshima ya chama, lazima baadhi ya matokeo ya uchaguzi wa jumuiya za chama na zile za mikoani na wilayani kulikokuwa na malalamiko ya rushwa, yafutwe.“Safari hii rushwa ilitumika vibaya sana kiasi cha kukitia aibu chama chetu. Namna bora ya kurejesha imani hiyo ni kufuta baadhi ya matokeo ya jumuiya, mikoa na wilaya, vinginevyo tutakuwa na wakati mgumu sana,” alisema mtoa habari wetu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoulizwa na gazeti hili endapo barua ya malalamiko kupinga ushindi wa uongozi mpya wa UVCCM, alisema hawezi kukataa wala kukubali kwani hajaiona na sio lazima barua hiyo aione.“Barua zote za malalamiko zinafika kwa Katibu Mkuu. Kwa hiyo kama ameipata kabla hajaleta kwenye vikao, siwezi kujua, “ alisema Nape.Akizungumzia kanuni za chama kuweza kufuta matokeo, Nape alisema hilo linawezekana kama chama kikijiridhisha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi ikiwemo suala la matumizi ya rushwa.
Katika uchaguzi wa UVCCM uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma na kutawaliwa na vitendo vya rushwa, mgombea Sadifa Juma Khamis aliibuka mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM taifa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Mboni M. Mhita.
Baadhi ya wajumbe waliongia NEC kupitia jumuiya hiyo ni pamoja na Jerry Slaa, Deo Ndegembi, Anthony Mavunde na Jonas Nkya.Mbali ya kudaiwa kushinda kwa rushwa, mwenyekiti huyo mpya tayari ameshakutana na changamoto nyingine kwamba amedanganya umri wake.Habari na
No comments:
Post a Comment