Na Rodrick Ray
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwasili wilayani Manyoni, mkoani Singida Jumatatu ya Novemba 5, mwaka huu kwa ziara siku moja.

Mkuu
wa wilaya ya Manyoni, Fatma Toufiq ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano
wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika mjini Manyoni.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo wakati wa ziara hiyo rais Kikwete atazindua na atafungua barabara ya Manyoni –Isuna ambayo imeshaanza kutumika,atazindua rasmi barabara ya Manyoni –Itigi-Chaya ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.

Bi
Toufiq amesema kutokana na ujio huo wa rais hivyo kila mmoja atachukua
nafasi yake kuhakikisha anahamasisha wananchi wake kufika kwa wingi
kwenye maeneo hayo kwa sababu hiyo ni miongoni mwa kazi kubwa ambazo
serikali imafanya.
Pamoja na mambo mengine yaliyofanywa na serikali, lakini mkuu wa wilaya huyo amezitaja baadhi kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara itakayofunguliwa jumatatu na kiongozi huyo mkubwa wa kitaifa.
Hata hivyo, Bi Toufiq amesema pamoja na kazi ya uzinduzi na ufunguzi,vile vile Rais atakuwa na mikutano ya hadhara kwenye maeneo ya Itigi na Manyoni

No comments:
Post a Comment