EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, November 5, 2012

Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu.

ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa yupo nchini Ujerumani kwa matibabu na uchunguzi wa kiafya.Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli jana hakuwapo katika uzinduzi wa mradi wa Barabara ya Minjingu hadi Arusha na shule jimboni kwake, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete aliye ziarani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga na baadaye kusambazwa kwa waandishi wa habari, Lowassa alieleza kusikitishwa kutokuwapo jimboni kwake wakati huo ambao Rais Kikwete anatembelea jimbo lake.Lowassa alisema kuwa, hali hiyo imetokana na kuwa safarini kwa ajili matibabu lakini akasema anaamini mambo yataenda vizuri si kwa ziara hiyo ya Rais Kikwete bali hata vikao vya juu vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.Katika taarifa hiyo, alimsifu  Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia  na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.

Katika maelezo hayo, Lowassa alieleza tatizo linalomsumbua kuwa ni macho, lakini pia atatumia nafasi hiyo kuchunguza afya yake.Aidha, alimshukuru Rais Kikwete kwa kuzindua miradi hiyo akisema inadhihirisha mambo mawili makubwa aliyoyafanya kwa kiwango cha juu chini ya uongozi wake akiwa Rais wa Tanzania.

“Mosi, chini ya uongozi wako shule nyingi zaidi zimejengwa kuliko awamu zote zilizotangulia. Pili, kilomita za barabara za lami zilizoongezeka wakati wa awamu yako ni ndefu kuliko wakati mwingine wowote,” alisema Lowassa na kuongeza:“Kwa hakika umetekeleza vizuri, kikamilifu na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, mwaka 2005 na 2010. Sisi wanachama wa CCM na wananchi wa Monduli ni mashahidi wa jambo hili. Tunaamini ndivyo ilivyo kwa nchi nzima.”Mwishoni mwa wiki ijayo CCM itafanya uchaguzi mkuu wa uchaguzi ngazi ya taifa kuanzia mwenyekiti wa chama na viongozi wengine, ili kukamilisha kupanga safu mpya ya uongozi kwa ajili  ya uchaguzi mkuu wa 2015.


CCM ipo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ambapo tayari jumuiya zake za Wazazi, Vijana na Wanawake zimekamilisha chaguzi hizo, huku kambi ya Lowassa ikitajwa kuibuka kidedea kwa kunyakua nafasi mbalimbali zilizowaniwa, kuanzia ngazi za wilaya hadi jumuiya za chama kitaifa.Katika uchaguzi wa UWT, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku wajumbe sita kati ya wanane  waliochaguliwa kuwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambi hiyo.
Wajumbe sita kati ya wanane walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC kupitia jumuiya hiyo  wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa,  huku mmoja akitajwa kuwa hana kundi lolote huku mwingine akitajwa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa UWT na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Killango Malecela.


Kwa upande wa UVCCM, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kura 483 na makamu wake, Mboni Muhita pia wanatajwa kuwa wafuasi wa kambi ya Lowassa.Waliotwaa ujumbe wa NEC na ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja huo, pia wanatajwa kuwa waumini wa kambi hiyo.

Hata hivyo, katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi uliokuwa wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili, waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na masilahi na makundi huku Martha Mlata akikataa kuzungumzia uchaguzi huo.

Rais Kikwete

Akizungumza katika hafla hiyo, Kikwete alisema kwamba ni lazima barabara zote ziwekwe matuta ili kuzuia ajali za barabarani, akieleza kuwa mara nyingi baada ya ujenzi wa barabara, kinachofuatia ni vifo vinavyotokana na tabia ya madereva wakorofi.Chanzo cha Habari ni Mwananchi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate