JUZI ilikuwa ni siku chungu kwa washiriki watatu wa Kijiji cha
Maisha Plus, baada ya kuondolewa kutokana na kupata kura chache za
kuwawezesha kuendelea kubaki.
Waliokumbwa ni washiriki Magreth Msechu wa Mbeya, Saad Mohamed Kilimanjaro na Hidaya Shaban kutoka Zanzibar.

Washiriki hao, ambao hawakuamini kama ndio ulikuwa mwisho wao wa
kuwania kitita cha sh milioni 20 za shindano hilo, walipata nafasi ya
kuzungumza kabla ya kuondoka.
Magreth na Hidaya, walipongeza hatua waliyofikia lakini kwa upande wa Saad, alishindwa kuzungumza lolote.
Kabla ya kutolewa washiriki hao, washiriki wengine waliokuwa kwenye
hatari hiyo ni Rashid Ndunduke, Bahati Kisula, Dorah Mhando, Swaumu
Shabani, Tatu Masoud, Gabriel Lwinga na Jonathan Joachim.
Nelly: Nimejifunza mengi
MSHIRIKI wa Kijiji cha Maisha Plus, Nelly Niyonhuru kutoka Burundi,
juzi alifunguka kwa kusema tangu afike kijijini humo amejifunza mengi
ikiwamo kuishi na watu wa makabila tofauti, ambapo kuna makabila makuu
matatu.
Nelly alisema, amejifunza kuteka maji kisimani, kupika chakula kwa
kutumia jiko la kuni na kulima, ambavyo hakuweza kufanya katika maisha
yake.
Mbali na Nelly, washiriki wengine nao walisema wamejifunza elimu za ujasiriamali na uchongaji wa vitu ndani ya kijiji hicho.
Wanakijiji hao walisema, watakwenda kuifanyia kazi elimu waliyoipata, hata watakapotoka ndani ya shindano hilo.
Vitu vyapotea dukani
WASHIRIKI 18 waliobakia ndani ya Kijiji cha Maisha Plus, wameanza
kujawa na hofu baada ya duka la Kijiji, kuondolewa vitu vyote muhimu
ukiwamo mchele, sukari, unga wa ngano na sembe.
Wanakijiji hao walipigwa butwaa kwa tukio hilo na kila mmoja hajui nini kitafuata.
Aidha, Jaji Mkuu wa Maisha Plus, Masoud Kipanya, atakuwa akitoa kazi maalumu kwa washiriki hao hadi siku ya mwisho.
No comments:
Post a Comment