WAKATI wanachama wa Simba wakihaha kutaka mkutano wa dharura, watani zao Yanga wao wameamua kuusogeza karibu mkutano wao mkuu.Mabingwa hao wa soka Afrika Mashariki na Kati, walikuwa wafanye
mkutano mkutano wao mkuu Desemba 16, lakini wameirejesha nyuma hadi
Desemba 8 katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Laurence Mwalusako, wamerudisha
nyuma mkutano huo kutokana na sikukuu za Christmas na mwaka mpya ili
wanachama wao wawe na muda wa kufanya maandalizi hayo.“Awali tulitakiwa kuufanya Desemba 16, tumerudisha nyuma ili kuwapa nafasi wanachama kujiandaa na sikukuu,” alisema Mwalusako.
Mwalusako, aliwaomba wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku
hiyo kujadili mambo mbalimbali yahusuyo klabu yao na mwenendo mzima wa
timu yao.
“Tutajadili mambo mbalimbali katika mkutano huo mkuu, ambao
tunatarajia kuufanyia Dar Live Mbagala, hivyo basi wanachama ni muda wa
kujipanga na kujitokeza katika mkutano huo ambao ni muhimu kwa timu
yetu,” alisema.Wakati Yanga mambo yakiwa shwari, watani zao Simba hali si shwari
kutokana na timu yao kuboronga, jambo linalosababisha hivi sasa baadhi
ya wanachama kutaka mkutano wa dharura ili kujadili hali hiyo.
No comments:
Post a Comment