KWA mara ya kwanza, warembo mbalimbali wanaoishi barani Ulaya
wanatarajiwa kushiriki mashindano ya Miss East Africa 2012
yatakayofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Desemba 7,
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Events, ambao ndio
waandaaji, Rena Callist, warembo hao ambao wameweza kushinda huko waliko
na kupata nafasi hiyo kushiriki Miss East Africa ni Cynthia Ikwene
(24), kutoka Ubelgiji, Mareg Marcos (21), wa Uholanzi na Fiona Ruboneka
(24), aliyetokea Ufaransa.
Callist alisema fainali za Miss East Africa 2012, zitashirikisha
warembo kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti,
Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoro,
Shelisheli, Mauritius na wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment