EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, November 10, 2012

MASWAI AJIMALIZA SPIKA ASEMA TUHUMA ZAKE ZILIKUWA ZA KUJIHAMI.

Na Ratifa Baranyikwa , Dodoma-Tanzania Daima.

KAMATI ndogo ya Bunge iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa, imemkaanga Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwa alidanganya kwamba baadhi ya wabunge walimwomba rushwa.
Pia ripoti hiyo, imebanisha wazi kuwa, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na wabunge watano walitoa tuhuma za uongo kwa wabunge wenzao ambazo walishindwa kuzithibitisha mbele ya kamati.
Akitoa taarifa ya kamati hiyo ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Hassan Ngwilizi, Spika wa Bunge Anne Makinda aliwataja wabunge hao kuwa ni Kangi Lugola (Mwibara-CCM), Ali Keissy (Nkasi Kaskazini-CCM) na Tundu Lissu (Singida Mashariki-CHADEMA).
Wengine ni Joseph Selasini (Rombo-CHADEMA), na John Mnyika wa Ubungo (CHADEMA) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.
Akisoma ripoti hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, Makinda alisema aliipa kamati hiyo hadidu moja tu ya rejea ambayo ni kuchunguza na kumshauri iwapo tuhuma kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli au hapana.

Matokeo ya Uchunguzi
Spika alisema kuwa Maswi aliandika barua yenye Kumb. Na. SBA. 88/223/01/28 kwenda kwa Katibu wa Bunge Julai 31, mwaka huu, akimtuhumu Mbunge wa Viti Maalumu, Sara Msafiri (CCM) kwamba Februari 6, mwaka huu alikwenda ofisini kwake mjini Dodoma na kumuomba rushwa ya sh milioni 50 kwa ajili ya kuwagawia baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, lakini kamati imembaini alizua tuhuma hizo.
Alisema kuwa kamati imebaini kuwa Maswi aliibua tuhuma hiyo kama njia ya kujihami dhidi ya tishio la wabunge wa CCM, Munde Tambwe (Viti Maalumu), Christopher ole Sendeka (Simanjiro) na Sara Msafiri (Viti Maalumu).
Makinda alifafanua kuwa katika ushahidi wake wa maandishi, Maswi alitamka kwamba wabunge hao walimweleza kuwa ni lazima aachie nafasi yake ya ukatibu mkuu, kwa kuwajibika kutokana na utendaji usioridhisha.
“Nakubali alitamka hivyo mbele ya Waziri Mkuu kwamba mimi sina sababu ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu sasa na mimi mtu akiniambia hivyo yeye kwanini aendelee kuwa mbunge?” alikaririwa Maswi katika mahojiano yake na kamati hiyo.
Spika alisema Maswi ameshindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya mbunge Msafiri.
Kuhusu Maswi kumtuhumu Mbunge wa Bukene, Selemani Zedi (CCM) kwamba alimuomba rushwa ya sh milioni mbili kwa kila mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kamati imebaini kwamba aliwazushia kwa nia ya kujihami dhidi ya tishio la kumng’oa.

Kamati pia imesema tuhuma zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini 2012/2013 kwamba baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wanajihusisha na vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kibunge kwa kupewa rushwa na makampuni makubwa ya mafuta ili wayatetee kuhusiana na zabuni ya ununuzi wa mafuta mazito kuendeshea mitambo ya IPTL, hazijathibitika.
Alisema kutokana na msimamo wa Sendeka na Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) wa kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya Waziri na Katibu Mkuu wake, kutokana na kukiuka sheria ya manunuzi baada ya kununua kwa dharura mafuta mazito kutoka katika Kampuni ya Puma Energy (T) Ltd, hali hiyo ilizusha shaka kwa baadhi ya wabunge.
Makinda alibainisha kuwa, wabunge Selasini, Lugola, Keissy, Vicky Kamata, walianza kuwatilia shaka wabunge hao kuwa huenda walikuwa wamepewa rushwa na makampuni ya mafuta.
Hata hivyo, Spika alisema kamati imebaini kuwa Selasini ameshindwa kuthibitisha kauli yake kwamba kulikuwa na makampuni ya mafuta yaliyokuwa Dodoma yakigawa fedha kwa wabunge kwa nia ya kushawishi yapatiwe zabuni.

“Mimi sina ushahidi wa moja kwa moja kwamba fulani kapokea rushwa, wabunge katika ujumla walikuwa wanatuhumu na sijui kama walikuwa na ushahidi au hawana,” alikaririwa Selasini.
Kuhusu Mnyika, ambaye katika hotuba yake ya Kambi ya Upinzani alisema kuwa kuna kampeni inafanywa ndani na nje ya Bunge ili uamuzi wa Maswi ubatilishwe kwa maslahi ya makampuni yaliyokosa zabuni, naye alishindwa kuthibitisha.
Mnyika alikaririwa na kamati hiyo akisema vyombo mbalimbali vya habari vimeandika vikinukuu wabunge kwa majina yao na kwamba mpaka anasoma hotuba yake bungeni hakukuwahi kuwa na kanusho la habari hizo.
Spika alisema Lugola, ambaye alisema kuwa kuna watu wameanza kutumia Bunge kwa kudhani wabunge wanakimbilia peremende na vipesa vyao ili kuhakikisha kwamba serikali inatekeleza matakwa yao na nchi haitawaliki kwa kukosa umeme, naye alishindwa kuithibitishia kamati.

Alisema Keissy naye alishindwa kuthibitisha juu ya tuhuma za rushwa alizozitoa ndani ya Bunge dhidi ya wabunge hao, na alipohojiwa na kamati alisema ushahidi wake ni wa kukisia na kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu lazima angejua kuna chochote.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo naye alipohojiwa na kamati kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni wakati akihitimisha hotuba yake ya bajeti, alishindwa kufanya hivyo.
Alipotakiwa kuithibitishia kamati juu ya madai ya makampuni hayo ya mafuta kuwepo Dodoma na kugawa fedha kwa wabunge, Prof. Muhongo alisema; “Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikukumbushe kwamba mambo yote ambayo mtakuwa mnayasikia kutoka kwangu na kutoka kwa wengine ambao mnahitaji kuwahoji yatakuwa ni allegations (tuhuma).”

Kuhusu kauli yake kwamba baadhi ya wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wana mgongano wa kimaslahi kwa kufanya biashara na TANESCO, akimtaja Msafiri kuingia mkataba wa kuiuzia TANESCO matairi - tuhuma hizo pia zilitolewa na Maswi na Lissu, alisema hazikuwa za kweli.
Katika uchunguzi wake, kamati baada ya kuchambua nyaraka zilizowasilishwa, ilibaini kuwa kampuni iliyoingia mkataba wa kuiuzia matairi TANESCO, inaitwa Shariffs Services and General Supply Limited ambayo kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usajili wa Makampuni (BRELA), Msafiri na Munde siyo wamiliki wala wanahisa wa kampuni hiyo.

Spika alisema kuwa kamati imebaini kuwa hakuna mahali popote katika hatua za mchakato wa zabuni ya kuiuzia TANESCO matairi ambapo wabunge waliotuhumiwa wamehusika.
Alisema kitendo cha Msafiri kufuatilia kusainiwa kwa mkataba ambao TANESCO ilikuwa imeupitisha kuchukua nakala na kumpelekea mhusika ambaye ni jirani yake si uthibitisho wa kutosha kwamba anafanya biashara ya kuliuzia matairi shirika hilo au yeye kuwa ndiye mmiliki.

Uamuzi wa Spika
Katika uamuzi wake, Spika alisema kuwa Maswi amelifedhehesha na kulidhalilisha Bunge kwa kuzusha tuhuma za uongo na kuufanya umma wa Watanzania uamini kwamba baadhi ya wabunge wanajihusisha na vitendo vya rushwa.
Kutokana na hilo, Spika alisema anampa onyo kali na kumtaka asirudie tena.
Aidha, Spika aliwatetea wabunge waliosema uongo, akisema kuwa walilisemea kwa nia njema ya kulikemea na hawakumtaja mbunge yeyote.
Hata hivyo, pamoja na nia njema ya wabunge hao, Spika aliwashutumu kwa kuzungumza mambo ambayo hawakuyafanyia utafiti kupata ukweli.
Spika alitoa onyo kwa wabunge hao na kuwataka wasirudie kosa hilo la kuvunja kanuni za Bunge na kuwataka wabunge waliotajwa na Tundu Lissu wamsamehe ili waanze ukurasa mpya.
Kuhusu Waziri Muhongo, Spika alimtaka awe muangalifu kwani anapotoa kauli bungeni huchukuliwa kuwa ni kauli za serikali.

Spika aliongeza kuwa, kutokana na uzito wa tuhuma hizo endapo matokeo yangethibitika angewasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua hatua.
Alisema suala hilo limewapa somo kutosema jambo lolote bila ya kufanya utafiti, na kuwataka wabunge wajizuie kusema tu ili mradi wasikike.
Kuhusu kamati iliyovunjwa, Spika alisema kuwa kwa sababu muda wa kuzibadili kamati umebaki mdogo, hana sababu ya kuirudisha kwa sasa.
Alisema katika mkutano ujao tayari kamati nyingine itakuwa imeundwa, lakini hawatakuwa wajumbe wale wale wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa kwa sababu hawataweza kufanya kazi pamoja wakati kukiwa na kutoelewana.

Maoni ya wabunge
Akizungumzia kuhusu matokeo ya ripoti hiyo, Msafiri alisema amefurahi kwani Watanzania sasa wameujua ukweli.
Alisema chanzo kilikuwa ni Maswi kwani lengo lake lilikuwa ni kuwagawa wabunge ili washindwe kuisimamia serikali.
Msafiri alifafanua kuwa, kitendo cha Maswi kutojibu hoja na kutaka kuwazima wabunge kwa milioni mbili zake ndicho kilichozusha yaliyotokea bungeni.
Naye Zedi, alisema kuwa yeye alikuwa na uhakika kwamba kilichokuwa kikisemwa ni uongo na ukweli ungedhihirika baada ya uchungunzi.
Alisema yeye amewasamehe wote waliomzushia na kama alivyosema Spika, yuko tayari kuwasamehe na kushirikiana nao katika kazi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate