Cirkovic, ameondoka nchini juzi usiku, kurujea kwao Serbia, baada ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo.Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, kocha
huyo hatarejea tena nchini kuionoa Simba, kwani imeishavunja naye
mkataba.

“Milovan aliingia mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha Simba
Juni mwaka huu na katika masharti ya mkataba wake, yule atakayesitisha
mkataba anapaswa kuulipa upande athirika mshahara wa mwezi mmoja mbele,
hivyo uongozi wa Simba tayari umemalizana naye,” kilisema chanzo hicho
huku kikigoma kubainisha sababu za kutemwa kwa Kocha huyo, aliyeipa
Simba mafanikio haraka haraka ikiwamo kutwaa ubingwa wa Bara.
Mtoa habari huyo, ambaye aliomba jina lihifadhiwa, alibainisha kuwa,
katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilichofanyika wiki
iliyopita, kiliamua kuwateuwa Talib Hilal kuwa Kocha Mkuu na Jamhuri
Kihwelu ‘Julio Alberto’ kukamata nafasi ya Meneja.
Hata hivyo, Julio alipoulizwa kuhusiana na uteuzi huo, alisema anasikia tu, ila hajapewa barua rasmi.
Julio alisema kuwa, hata hivyo hawezi kukubali kuifundisha klabu hiyo
hadi atakapokaa na uongozi wa Simba kuupitia mkataba wake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alithibitisha
kuondoka kwa Cirkovic, lakini akidai amekwenda kupumzika.
"Tayari Kocha Milovan amekabidhi taarifa yake ya mzunguko wa kwanza wa
ligi na ameshaondoka kwenda kusalimia familia yake nchini Serbia,
"alisema Rage huku akishindwa kuweka wazi kama atarejea ama ndo moja kwa
moja.
Simba imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya
tatu, baada ya kujikusanyia pointi 23 ikiwanguliwa na Azam FC pointi 24
na Yanga pointi 29.
No comments:
Post a Comment