Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’.
Na Musa Mateja
MUDDY Suma ndiye mmliki wa gari aina ya Toyota Harrier namba T 478 BVR ambalo lilipinduka na kusababisha kifo cha staa wa vichekesho Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ ameibuka na kusema machache ambayo Watanzania wengi wangependa kujua kutoka kwake.

Akizungumza jana na paparazi wetu msibani Kijiji cha Lusanga, Muheza,
Tanga, mmiliki huyo alisema haikuwa mara ya kwanza kwa Sharo Milionea
kuazima gari kwake na kwenda nalo Muheza kisha kurudi salama Dar es
Salaam.
“Hii si mara ya kwanza kwa jamaa (Sharo Milionea) kuazima
gari langu, ameshaenda nalo mara ya kwanza na alirudi salama, sasa hii
mara ya pili ndiyo yametokea hayo,” alisema.
Akaongeza: “Lakini pamoja na yote hayo ni ajali tu, mi namwachia Mungu. Hakupenda yamfike yaliyomfika, ila nashukuru gari langu lina bima kubwa najua hakijaharibika kitu.”
Wakati huohuo kumekuwa na utata kwamba, marehemu alitoka Dar na gari lake hadi Kitongoji cha Hale kilichopo Barabara kuu ya Segera Tanga ambapo ndipo alipochukua Harrier hilo, lakini ukweli ni kwamba gari hilo alitoka nalo Dar.
Marehemu Sharo Milionea amezikwa saa 7 mchana jana kwenye makaburi ya Kijiji cha Lusanga, Muheza, Tanga ambako pia ndiko alikozaliwa.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

No comments:
Post a Comment