Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari
kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River
pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya
Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani.
PICHA NA IKULU
Baadhi
ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za
uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu
wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania
Rais Jakaya Kikwete akitoaa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya
ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi
wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa
104.4 kwa upande wa Tanzania
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya
ya Afrika Mashariki wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa
barabara hiyo kwa kukata utepe.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya
ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali
waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
No comments:
Post a Comment