Habari imeandikwa na Rodrick Mushi
Akizungumza kwa shida akiwa amelazwa hospitali ya St Joseph iliyopo Mjini hapa Ndagula alisema kuwa aligongwa na gari dogo aina ya Toyota Rava4 yenye namba T 265 AUE.
Ndagula alisema kugongwa kwake kumekuja baada ya kupata taarifa kwa mtoa taarifa ya kuwepo magari zaidi ya 12 ambayo yalikuwa yamepakia sukari, tayari kwa ajili ya kwenda Kenya kwa kupitia njia za panya Wilayani Rombo.
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo akiwa na mwandishi mwenzake wa Mwananchi,Daniel Mjema,walianza kufuatilia magari hayo kupitia njia ya Holili kuelekea Rombo ikiwa ni majira ya saa 6:00 usiku.
Walipopita eneo la Holili kuelekea Rombo eneo ambalo linachimbwa udongo wa ‘pozolana’ ambao unatumika kutengenezea sementi ndipo walipokutana na magari mawili yakiwa na sukari aina ya fuso yenye namba T 288BHF na lingine likiwa na namba T280 BUZ.
Alisema baada ya kuona magari hayo yakiwa na sukari walimtaarifu kamanda wa Polisi Robert Boaz kumueleza kilichokuwa kinaendelea.
Wakati wakiwa bado katika eneo la tukio wakiendelea na kazi,ambapo zaidi ya magari nane yakiwa na sukari yalikuwa yamekwishapita, ndipo ilifika gari ndo,aina ya Toyota RAV4 yenye namba T265 AUE na kupaki mbele ya alipokuwa amesimama Ndagula.
Alisema kuwa akiendelea kuandika namba za magari yaliyokuwa yanapita,ikiwemo pamoja na gari ndogo ambalo linasadikiwa kuwa mmoja wa wafanyabishara mwenye mzigo huo wa magendo.
“Wakati nikiwa nimesimama mbele ya gari dogo,ndipo mtu mmoja alitoka kwneye magari mawili yalikuwa yamepaki na kuingia kwenye gari dogo na kunifuata nilipokuwa na kunigonga na kuanguka”Alisema Ndagula.
Hata hivyo alisema kuwa kilichosaidia ni kuliona gari dogo wakati likimfuata kwa makusudi kwa lengo la kumgonga na kulikwepa lakini likamuumiza sehemu mbalimbali za mwili.
Hata hivyo jitihada za kumtafuta kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro,Robert Boaz kudhitisha tukio hilo zimeshindikana baada ya kupiga simu yake ya mkononi bila kupatikana.
Swali la kujiuliza ni kwamba Polisi wetu na viongozi wa usalama wanafanya kazi gani kama watu wachache kwa maslahi yao binafsi wanaamua kuvunja sheria zilizowekwa na hili siyo kwamba wamekuwa hawafahamu la hasha biashara ya megendo ipo na inaendelea kufanyika kila kukicha.
No comments:
Post a Comment