Rais Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa hadhara mjini Iowa huku Wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu ya White House.
Wagombea urais nchini Marekani, Barack Obama (kulia) na Mitt Romney. |
Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkali.
Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment