RAFA Benitez ameteuliwa kuwa meneja wa Chelsea, akimrithi Roberto Di Matteo.Chanzo cha habari na Saluti5 www.saluti5.com

Mtaliano
DI Matteo alionyeshwa mlango wa kutokea asubuhi iliyopita licha ya
kuiongoza Blues kutwaa kombe Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA msimu
uliopita.
Bosi wa zamani wa Liverpool, Benitez, ambaye amekuwa nje ya kazi tangu alipokuwa na miezi 6 mibaya kwa Inter Milan mwaka 2010, anakuwa meneja tisa katika zama za Roman Abramovich ndani ya Chelsea. Atakutana na wachezaji kesho asubuhi (leo).
Chelsea imesema "mmiliki na bodi wanaamini kwamba Benitez ana uzoefu mkubwa ambao unaweza ukasaidia kutimiza malengo ya klabu kwa haraka"
No comments:
Post a Comment