Wizara ya Mashauri ya Nchi za
Nje ya Uingereza imeonya kwamba uwezekano unazidi kwamba kutatokea
mashambulio ya kigaidi katika eneo la Sinai nchini Misri; na imezidisha
uzito wa onyo hilo kutoka la kawaida na kuwa kubwa zaidi.
Ilani hiyo imetolewa kutokana na taarifa za hivi
karibuni kuhusua ile inayosemekana kuwa njama ya al-Qaeda na kupatikana
kwa silaha katika eneo hilo la Sinai.Piya linafuata polisi wa Misri kugundua kikundi
cha magaidi mjini Cairo, na baadhi ya taarifa zinaeleza magaidi hao
wakipanga kushambulia watalii kutoka mataifa ya Magharibi.
Hata hivyo Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya
Uingereza inasema hali katika maeneo ya watalii ya Bahari ya Sham,
pamoja na Sharm el Sheikh, ni tulivu.
No comments:
Post a Comment