WAKATI zimebaki dakika chache kabla ya jijini la Dar es Salaam,
kutoka katika mfumo wa analojia na kuingia katika mfumo wa dijitali,
zaidi ya kaya 30,000 kukosa mawasiliano kwa njia ya luninga na redio
baada ya mitambo ya kurusha mawasiliano kuzimwa rasmi kuanzia saa 6:00
usiku huu.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa imebaini kwamba zaidi ya kaya 30,000 jijini Dar es Salaam,hazikufanya
maandalizi ya kununua ving’amuzi kwa ajili kuuangalia matangazo ya Redio
na Lninga,ambapo maeneno yatakayokumbwa na mabadiliko hayo ni pamoja
Mbagala,Gongo la Mboto,Tegeta,Kigamboni pamoja Kisarawe.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imefikia hatua ya Tanzania
kuungana na nchi nyingine duniani kuanza kurusha matangazo ya
televisheni kwa mfumo wa Dijitali zikiachana na ule wa Analojia. Shirika
la Kimataifa la Mawasiliano (ITU), limezitaka nchi zote duniani kuhamia
kwenye mfumo huo wa kurusha matangazo ya televisheni wa dijitali kutoka
mfumo wa analojia ifikapo Julai 2015.
Ikiwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC),
Tanzania imeanza kutekeleza azimio la nchi hizo ilizozitaka kufanya
hivyo mwaka huu wa 2012, badala ya kusubiri hadi tarehe ya mwisho
iliyowekwa na ITU. Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele kuhamia kwenye
mfumo huo wa dijitali, ingawa kwa mtindo wa awamu, nchi nyingine
wanachama wa EAC hasa Kenya na Uganda bado hazijaingia katika mfumo huo.
TCRA imezikabidhi kampuni tatu kufanya kazi ya usambazaji wa mfumo
huo wa dijitali, ambazo ni Basic Transmissions inayoundwa na Kampuni za
IPP Media na Sahara,Communications, Kampuni ya Ting ya Agape Associates
na Star Media Tanzania Limited (Startimes) ambayo ina ubia na Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Communications and Technology ya
China.
TCRA imekuwa ikielezea kuwa Tanzania ipo tayari kujiunga na
mfumo huo kwa kuwa asilimia kati ya 22 kati ya 24 ya nchi ambayo
inatumia analojia, tayari imefikiwa na mtandao wa mfumo wa dijitali,
ikijumuisha miji minane ambayo kwa kiasi kikubwa kampuni ya Startimes
imeifikia.
No comments:
Post a Comment