KWA
mujibu wa orodha iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Brazil,
katikati ya wiki, Kocha wa Real Madrid ya Hispania, Mreno Jose Mourinho
ndiye anayeongoza kwa kutengeneza fedha nyingi, miongoni mwa makocha wa
soka duniani.
Kampuni
ya ushauri wa kibiashara ya Pluri Consultoria ya Brazil imetoa orodha
ya makocha 30 wanaotengezea fedha nyingi zaidi katika soka, ikimtaja
Mourinho kuingiza pauni milioni 12.3 kwa mwaka.
Carlo Ancelotti, anashika nafasi ya pili kutokana na mshahara wa pauni milioni 10.9 anaovuna Paris St. Germain.
Alex Ferguson wa Manchester United – ndiye kocha anayelipwa zaidi katika Premier League akikunja pauni milioni 7.6 kwa mwaka, huku akikamata nafasi ya nne katika orodha.
Kocha
wa England, Roy Hodgson ametupwa nafasi ya 30 akiingiza mshahara wa
pauni milioni 2 kwa mwaka, sambamba na Joachim Low wa Ujerumani na
Martin O’Neill wa Sunderland.
Harry
Redknapp anaingiza pauni milioni 3.2 kama ujira wake wa mwaka QPR na
amewekwa nafasi ya 14 akimwacha nyuma mrithi wake Spurs, Andre
Villas-Boas.
Kocha
wa timu ya taifa anayelipwa zaidi kuliko wengine ni bosi wa zamani wa
England, Fabio Capello, ambaye kwa sasa anainoa Russia. Huyu anakamata
nafasi ya saba akikusanya pauni milioni 6.3.
Orodha ya makocha hao 30 na fedha (paundi za Uingereza) wanazovuna kwa mwaka kwenye mabano hawa hapa;
1. Jose Mourinho – Real Madrid (£12.3m)
2. Carlo Ancelotti – Paris St. Germain (£10.9m)
3. Marcelo Lippi – Guangzhou (£8.7m)
4. Sir Alex Ferguson – Manchester United (£7.6m)
5. Arsene Wenger – Arsenal (£7.5m, pictured right)
6. Guus Hiddink – Anzhi (£6.7m)
7. Fabio Capello – Russia (£6.3m)
8. Tito Vilanova – Barcelona (£5.6m)
9. Jose Camacho – China (£4.8m)
10. Roberto Mancini – Manchester City (£4.8m)
11. Frank Rijkaard – Saudi Arabia (£4.3m)
12. Jupp Heynckes – Bayern Munich (£4.2m)
13. Andre Villas-Boas – Tottenham (£3.6m)
14. Harry Redknapp – QPR (£3.2m)
15. Jorge Jesus – Benfica (£3.2m)
16. David Moyes – Everton (£2.9m)
17. Manuel Pellegrini – Malaga (£2.9m)
18. Paulo Autuori – Qatar (£2.9m)
19. Abel Braga – Fluminense (2.8m)
20. Luciano Spaletti – Zenit (£2.7m)
21. Antonio Conte – Juventus (£2.4m)
22. Cesare Prandelli – Italy (£2.4m)
23. Vanderlei Luxemburgo – Gremio (£2.4m)
24. Muricy Ramalho – Santos (£2.4m)
25. Tite – Corinthians (£2.4m)
26. Ottmar Hitzfeld – Switzerland (£2.1m)
27. Joachim Low – Germany (£2m)
28. Marcelo Bielsa – Athletic Bilbao (£2m)
29. Martin O’Neill – Sunderland (£2m)
30. Roy Hodgson – England (£2m)
No comments:
Post a Comment